Niyongabire Eric, Maarufu Nipo Simple

Msanii huyo jina lake halisi ni Niyongabire Eric maarufu Nipo Simple. Alizaliwa bila miguu na mkono mmoja.

Anaeleza kwama hali hiyo ya ulemavu ilisababisha baba yake kumufukuza mama yake.

Ameeleza kwamba aliisha katika maisha magumu sana ya utotoni lakini kwa sasa anafanya kazi katika shirika linalowasaidia watoto walemavu. 

Kubwa zaidi Eric ni muimbaji na muigizaji katika filamu. Kulingana na yeye maisha ya awali yalimpiga chenga zaidi kwani hayakuwa mepesi "Baba yangu alinikata kwa sababu ya ulemavu wangu,' alisema

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

WAkati huo ameelezea kwamba anapitia unyanyapaa kutoka kwatu wengine katika jamii hasa anaenda sehemu ambayo yeye ni mgeni au hajakutana na watu wa sehemu hiyo.

"Watu wanaoishi mbali na kwetu, wakiniona tu hushituka  utafikiri kuna kitu cha ajabu ambacho kimetokea.  Baadhi yao wananishangaa sana, wananitizama kama kitu cha ajabu," alisema

Baba alimchukia mama kwa sababu amemzaa mtoto kiwete mwenye ulemavu, wakaachana wakapeana talaka kwa sababu yangu. Nimekuwa katika maisha magumu sana niliwaita watoto wenzangu baba.

Mwanamziki huyo ambaye alizaliwa na ulemavu mkubwa alikiri kwamba changamoto kubwa katika maisha yake ilikuwa wakati wa kupata mke.

Kuna wale walionikubali na wengine walinikataa. Sio rahisi kwa sababu unapoishi na ulemavu na hata nyinyi mnafahamu kwamba ni tatizo. Tunaishi vizuri na mke wangu. Walosema walisema hata baada ya kuijfungua. Walisubiri waone kama nitapata mtoto mlemavu," aliweka wazi mwanamziki huyo.