Mbunge wa Gatundu Kusini Gathuka Gabriel Kagombe alisema kuwa aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua anajigamba kupita kiasi na ufuasi mkubwa kutoka Mlima Kenya.
Akizungumza katika mahojiano na Kituo kimoja nchini kinachotangaza kwa Lugha ya mama mnamo Machi 18,2025 Kagombe alisema kuwa mazoea na tabia ya bwana Gachagua kujipiga kifua na kujigamba kutokana na uungwaji mkubwa wa eneo la Mlima Kenya ni wa kupitiliza sana na kukanusha kuwa si kweli anavyojinadi.
Kulingana na usemi wa Bwana Kagombe alisema kuwa Bwana Gachagua alijipa mamlaka ya kuzungumzia watu wa Mlima Kenya pasi kuchaguliwa na Wazee wa Jamii ya Gikuyu hivyo yeye anatangaza ufalme wake binafsi.
‘’Bwana Gachagua anataka kushikilia msimamao kuwa nafasi anayoishikilia ni ya manufaa ya Jamii ya Gikuyu na akumbuke hiyo nafasi hajapewa na Wazee wa Gikuyu hivyo anajitanua na kupiga injili yake peke yake kwa kujipandisha hadhi ya Kiwango cha kuwa msemaji wa jamii ambapo si hivyo’’Kagombe alisema.
Bwana Gachagua siku ya Jumatatu Machi 17,2025 alisema kuwa mchango wake katika kampeni za mwaka wa 2022 zilizaa matunda na zilikuwa za hali ya juu kuwashawishii wananchi hadi ikafikia uamuzi wa yeye kuteuliwa kama Naibu wa Rais .
Gachagua aliweza kueleza kwa kusema kuwa kutokana na usemi wake mwema na kuwaongelesha raia vyema hadi kufikia kiwango cha kumwamini na alipokuwa akiwaambia wananchi kuhusu mchakato wa uongozi ambao ulimpa uwezo wa kuwa kiongozi wa pili katika taifa.
‘’Tangu mwanzo Rais Ruto alifahamu wazi kuwa mimi si kiongozi wa’ Yes Sir’ lakini bado aliniteua kuwa naibu wake kutokana na ushawishi niliokuwa nao kwa wananchi hadi kuweza kunikweza na kufanya mimi kuwa kiongozo mkuu kiwango cha naibu wa Rais''.
Bwana Gachagua Katika mahojiano hayo aliweza kuzungumzia uzinduzi wa Chama chake kipya akisema kuwa mipango yote ilikuwa sawa na kuwa hivi karibuni kitaweza kuzinduliwa ambapo dereva atakuwa ni Gachagua Mwenyewe alisema.
‘’Watu wana uchu na ari ya kujua jina la chama chetu Pamoja na nembo na rangi kwa Jumla katika Mwezi wa tano hapo ndipo mbivu na mbichi itabainika tutaweza kuwaondoa wanachama kutoka chama cha UDA na kujiunga na chama chetu kipya’’ bwana Gachagua alisema.
‘’ Tungependa kuziomba Jamii zingine ziungane na sisi tutazipa nafasi za uongozi katika serikali kufikia sasa viongozi wengine tayari wana vyeo kwa hivyo tunaomba wale wengine waje upesi wapewe nafas katika meza ya mazungumzo’’ bwana Gachagua alisema
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!