Klabu yaomboleza mchezaji aliye hai

KLABU ya Arda Kardzhali ya Bulgaria imeomba msamaha baada ya kukaa kimya kwa dakika moja kwa mchezaji wa zamani ambaye bado yuko hai.

Wachezaji wa vilabu vya Arda Kardzhali na Levski Sofia walijipanga kwa mkono kwenye duara la kati kabla ya sare ya 1-1 Jumapili kwenye ligi kuu ya Bulgaria, wakiinamisha vichwa vyao kwa dakika moja kumuenzi mchezaji wa zamani, Petko Ganchev.

Walakini, iliibuka haraka kuwa Ganchev hajafariki na Arda Kardzhali walipotoshwa na chapisho la Facebook lililotangaza kifo cha mchezaji huyo wao.

Kosa lilipatikana wakati wa mchezo na kilabu kilituma ujumbe kwa mtandao wa runinga unaotangaza mchezo huo kuomba radhi wakati wa mapumziko.

Taarifa hiyo ilisomeka: "Ndugu waandishi wa habari na mashabiki wa timu ya Arda.”

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Uongozi wa PFC Arda ungependa kutoa pole nyingi kwa mwanasoka wa zamani wa timu hiyo, Petko Ganchev, na wapendwa wake, baada ya klabu kupata taarifa zisizo sahihi kuhusu kifo chake.

 

"Tunatamani Petko Ganchev miaka mingi ya afya na kufurahia mafanikio ya Arda."

Chapisho hilo lilionekana kufutwa kufikia Jumatatu jioni.

Sare hiyo ina maana kwamba Arda wako katika nafasi ya tano kwenye jedwali la timu 16 na bado anaweza kupata nafasi ya kucheza soka la Ulaya msimu ujao.

Levski wanasalia nafasi ya pili, lakini wako pointi 12 nyuma ya viongozi wa Ludogorets.