Hamisa Hassan Mobetto
Mwanamuziki na muigizaji nchini Tanzania Hamisa Mobetto amedai kwamba wapenzi wake wa zamani bado wanamwandama licha ya kufanya harusi na kutangaza hadharani kwamba yupo kwenye ndoa kwa sasa.

Mobetto akizungumza na na wanahabari ameeleza kuchanganyikiwa na mambo ya watu wa kiume kuendelea kumutafuta wakati wanajua kabisa yuko ndani ya ndoa.

"Mimi sijui ni bahati ama kero. Ama ni kwamba watu wanaonanga hawakukutendea haki, au sijui nini. Lakini wakati mwingine watu wanarudi kwa maisha yako kuangalia kama wewe bado ni mjinga. ukweli wakati mwingi mtu anarudi kuona kama bado mtu ni mjinga," alisema Mobetto.

"Sasa hivi akili zimekua lakini watu ambao tuliachana nao wananisumbua sana na si jambo la kufurahisha ni baya," aliendelea.

Muigizaji huyo pia ametupilia mbali maneno kwamba watu ambao wanarudi kwake kumutafuta wanampenda akisisitiza kwamba iwapo kungekuwa na mema au mazuri kati yao basi mahusiano yangekuwa yangalipo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

"Kungekuwa kuna jema katika yale mahusiano ama kama kungekuwa na mipango basi tungekuwa  bado tuko pamoja. Hakuna mwanamke ambaye anapenda kuhangaika mara hapa kisha hapa sio sifa nzuri. Lakini kama wakati tukiwa pamoja hatuuishi vizuri, yalishindikana ukaondoka hakuna kingine cha kutuleta pamoja, " alisisitiza mwanamziki huyo.

Hamisa Mobetto kwa sasa yupo Kwenye Ndoa na Mwanasoka Stephane Aziz Ki ambaye ni mzaliwa wa Bukina Faso. Mchezaji huyo kwa sasa anaichezea timu ya Yanga Star ilioko nchini Tanzania anakocheza kama mshambuliaji na kuvalia jezi nambari 10.

Baadhi ya wapenzi wa zamani wa muigizaji Hamisa Mobetto ni pamoja na mwanamziki maarufu wa bongo fleva Diamond platinumz ambaye pia walifanikiwa kupata mtoto naye mwaka wa 2017.

Awali Mobetto alikuwa katika uhusiano na Francis Ciza na wakafanikiwa kupata mtoto wa kike kwa jina  Fantasy Majizzo.

Mnamo Septemba 2021, kulikuwa na madai kuwa Mobetto  alikuwa katika uhusiano na rapa wa Marekani Rick Ross ila hakuna aliethibithisha uvumi huo baina yao wawili.

Mwanadada huyo alizaliwa Mwanza, Tanzania tarehe 10 Desemba 1994 katika familia ya Kiislamu na alikuwa na shauku ya kuwa mwanamitindo akiwa mtoto. Alifuata kazi yake ya uanamitindo baada ya kumaliza shule ya upili.