Mefnac ni dawa ya kutuliza maumivu

Bodi inayosimamia dawa nchini zikiwemo na dawa za sumu,''pharmacy and poison body'' ( PPB) imefutilia mbali maamuzi yake ya awali ya Desemba 12,2024 ya marufuku kwa dawa za kupunguza uchungu wa haraka.

Katika taarifa yake mnamo siku ya Jumatatu  17,2025 bodi iliweza kusema kuwa kutokana na utafiti wa kina wa  dawa aina ya Mefnac Oral aina ya tembe za kumezwa sasa imeafikia viwango vyake vinavyostahiki.

‘’Bodi ya famasia na dawa za sumu imeondoa ile amri ya mwanzoni iliyokuwa imepiga marufuku utumizi wa aina ya dawa za vidonge  kwa jina Mefnac Oral mnamo Desemba 11,2024 tembe hizo ambazo hutengenezwa na kampuni ya  dawa ya Efroze kutoka Pakistani".

Uamuzi huo ulijiri baada ya utafiti mkubwa  na ukaguzi wa kina kutekelezwa ambapo iliweza kuafikia vipimo sitahiki vya Diethlene Glycol DEG/ Ethilini Glycol EG,matukio ya vipimo yaliweza kudhibitisha hayo yote na kushauri kuwa sasa tembe hizo zilikuwa salama kwa matumizi ya binadamu.

Desemba 11,2024 bodi inayosimamia dawa nchini Pamoja na dawa za sumu iliweza kupiga marufuku utumizi wa dawa za vidonge kwa matumizi yoyote ya umma kwa kusema kuwa hazikuwa salama wala hazikuwa zimeaafikia viwango vyote vya ukaguzi vinavyotakikana na  kisheria Pamoja na bodi kwa jumla.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

‘’ Bodi ya ukaguzi wa dawa na sumu iliweza kutoa  taarifa kwa umma ikisema kuwa bodi ya udhibiti wa dawa nchini ingependa kufahamisha umma na watumizi wa vidonge au tembe aina ya Mefnac Oral kuwa imesitisha na kuharamisha matumizi yake ikiomba umma kuepuka kunu ua dawa hizo’’taarifa ilisema.

Uamuzi huo uliweza kuchukuliwa kufuatia hatari ambayo bodi hiyo ilikuwa imepata kutoka  kwa dawa hizo ambazo ilisema kuwa zilikuwa na viwango vikubwa vya kemikali aina ya Diethline Glycol na Ethylene ambayo ni hatari kwa matumizi ya binadamu.

Dawa hizo za Mefnac oral hutumika katika kutibu Kuumwa na kichwa,maumivu makali, kuumwa na meno,kuumwa na mishipa na wakati wa hedhi ili kupunguza maumivu zaidi.

Kwa kipindi cha muda huo pia bodi iliweza kubaini fika kuwa kulikuwepo na aina ya famasia au a  maduka ya dawa ambayo hayana  vibali rasmi vya kuendesha  biashara  ya uuuzaji wa dawa pamoja na leseni maalumu kutoka kwa bodi ya dawa nchini au mamlaka husika.

Bodi pia iliweza kubaini kuwa Desemba 2024 kulikuwepo na aina ya dawa kwa jina  Floracil 1000 fluorouracil 1000mg /2ml ya kudunga watu ambayo pia ilikuwa ni kinyume cha sheria madukani hivyo kuyaonya maduka ya dawa dhidi ya kuuza dawa hizo wakiwemo wananchi pia kutumia ikisema ilikuwa ni hatari  kwa maisha yao.