
Mwanaharakati wa masuala ya kijamii na Mwanamziki maarufu Tanzania, Agness Suleiman ambaye anajulikana kwa jina la Usani kama Aggy Baby sasa anadai kwamba hajawahi kutana na mwanaume ambaye kwa mwonekano wake anaweza kumudu mahari ambayo anahitaji.
Aggy Baby akizungumza na mwanahabari amepuzilia mbali uwezekano wake wa kuolewa na mchezaji wa mpira huku akidai wengi wao sura zao hazimpendezi.
"Mimi siwezi olewa na mchezaji mpira. Hata akuwe na ngamia 100, siwezi, bado sijaona. Sababu wengi kwanza hawana sura nzuri, sura zao ni za kipekee. Kwa ufupi siwezi kuolewa na mchezaji mpira. Kwa watu maarufu pia naona hawajafikia levo yangu. kama wasanii hawawezi kufikia mahari ambayo mimi naitaka, sijaona," alisema Aggy Baby.
Mwanamziki huyo pia amesisitiza kwamba kando na mali lazima mwanaume atakayemuoa awe na sura nzuri na kufurahia kuwa na yeye bilia uwoga na kwa furaha.
"Nitakaaje na mtu ambaye hana sura, haiwezekani, nitakuwa najikubaliaje nikiwa naye, Mbali na mahari, mbali na Ngamia pia angalau awe na sura nzuri. ila kwa watu wa mpira sijaona mtu na sura inayonipendeza,' alisema.
Aggy Baby kwenye mafanikio yake aliwahi kutambuliwa na kushinda tuzo ya watu 100 bora waliotambulika Afrika kutokana na juhudi zake za kutetea haki.
Mwanadada huyo alishinda tuzo yake kupitia taasisi yake ya Tupaze Sauti Foundation baada ya kutangaziwa kama mshindi kipengele cha ‘Notable in community Development’ katika tuzo za ‘100 Most Notable Africans Awards’ zilizofanyika nchini Rwanda.
Hivi karibuni, Agness alipata Tuzo ya Wanawake Maarufu Afrika 2024 (Most Notable Women in Afrika 2024) katika masuala ya familia na maendeleo ya jamii. Tuzo hii imemfanya kuwa mmoja wa watu 100 mashuhuri barani Afrika.
Kabla ya tuzo hiyo mwaka 2023 alipata tuzo ya mmoja ya watu 100 wa juu waanzilishi wa NGO. Alipata tuzo hiyo kwa kutetea na kuleta mabadiliko katika maisha ya watu kwenye masuala ya usawa wa jinsia, ukatili dhidi ya watoto, elimu, afya, uwezeshaji wanawake, haki za binadamu na maendeleo ya jamii.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!