Katika kipindi cha Patanisho kwenye stesheni ya Radio Jambo, jamaa kwa jina Steven kutoka Kitale aliomba kupatanishwa na mkewe ambaye walikosana baada ya kukaa kwenye ndoa ya miaka 3.

Gidi na Ghost kwenye Patanisho

Steven alieleza kwamba anahisi kabisa yeye ndiye alimkosea mkewe kwa hulka yake ya kukurupukia simu yake kila mara ilipokuwa inapigwa.

Alisema kwamba kila mara simu ya mkewe ilipokuwa inapigwa, alikuwa anataka kujua ni nani huyo aliyekuwa anampigia, jambo ambalo lilionekana kumkasirisha mkewe.

“Tulikuwa tunaishi kwa ndoa miaka 20, tulianza kuchumbiana 2021 tukakuwa tukivurugana tu mambo ya simu. Mtu akimpigia nilikuwa nataka kujua ni nani anampigia na kwa kweli mimi ndiye nilikuwa mwenye makosa. Hilo ni kama lilimkasirisha. Alitoka yuko mahali anafanya kazi na huwa tunaongea lakini nahisi nilimkosea nataka ajue kwamba bado nampenda,” Steve alisema.

Betty Wanyonyi kwa upande wake alithibitisha kwamba ni kweli tabia ya mumewe kurukia simu yake ndiyo iliyomfanya kuchukua uhusiano wao na kutaka kuivunja.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Mimi ni yule ninauza kwa duka, mteja akipiga simu kuulizia kuhusu bidhaa huyo mume wangu anaanza kuhisi kwamba ninamsaliti katika mapenzi. Kila wakati mwenye anapigac simu anataka kuona ni nani na hicho ndicho kilinifanya nikakasirika.

“Hata kama kuna wale wateja ambao wanajaribu kunitongoza nilikuwa nawaambia kwamba nimeolewa,” Betty alijieleza.

 “Nataka tu kukuomba msamaha na hata hayo mambo ya simu sitawahi shika simu yako hata siku moja,” Steven alinyenyekea akisisitiza kuikwepa kabisa simu ya mpenziwe.

Baada ya tathmini ya muda, Betty alitamka kwamba amemsamehe huku Steven akieleza furaha yake baada ya kusamehewa na mpenzi wake.