Matukio ya amri ya Kunyongwa kwa Mkenya Margaret Nduta Macharia aliye na umri wa Miaka 37 kule Vietinamu ilibuua hisia na uangalifu mkali kuhusu sheria za nchi za Ulaya kuhusu ulanguzi wa Dawa za Kulevya.

Nduta alishikwa  mnamo Machi, 6 2025 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo mbili za mihadarati aina ya Kokeini kutumia uwanja wa ndege wa Tan Hati Nhat katika mji wa Chi Minh

Kesi ambayo imezuiwa kutokana na wito wa kidiplomasia hali iliozua tumbo joto kuhusu msimmao mkali wa kisheria ambao nchi ya Vietnam huchukua dhidi ya walanguzi wa dawa za Kulevya.

Nchi hiyo iliyo na  sheria kali ambazo usipozingatia huenda makuu yakakufika yakiwemo kunyongwa kwa mfano na baadhi ya  sheria na masharti  ambayo taifa hilo huweka kuzingatia  ni kama.

Kifo dhidi ya usafirishaji wa dawa za Kulevya  nchi hiyo huweza kuwa na sheria kali dhidi  ya ulanguzi wa dawa za kulevya duniani kote.Kulingana na sheria za nchi hiyo usafirishaji wa Gramu zaidi ya 600 za hiroini au zaidi ya kilo 2.5 huweza kusawasishwa na mtu Kunyongwa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika Kesi ya Nduta mafisa wa Ukaguzi waliweza kubaini kuwa  zaidi ya kilo 2 za kokeini zilizokuwa zimefichwa ndani ya begi lake  zilipatikana, licha ya yeye kusisitiza kuwa hakukuwa na ufahamu wa dawa hizo kupatikana katika mkoba wake ila maamlaka ilimueleza kuwa mapuuza si utetezi na sheria za Vietianamu dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya zingechukua mkondo wake ipasavyo.

Uhalifu mwingine ni Kunyongwa kwa kupatikana kama umejidunga dawa zizo hizo za kulenya mataifa mengi yanapozidi kuachana na sheria hiyo taifa la Vietinamu lingali limeshikilia msimamo huo wa kunyonga watu .

Tangu mwaka wa 2013 taifa hilo limebadilisha mtindo uliokuwepo wa kupigwa risasi na badala yake likakumbatia  mtindo wa kunyonga,licha ya kuwepo kwa shinikizo nyingi kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu kurai taifa hilo kuuasi mtindo huo bado taifa la Vietinamu lingali limeshikilia mkondo huo kuhusu kunyonga watu.

Kulingana na kujitetea kwake bi Nduta alisema kuwa kupitia kwa mawakili wake kuwa mwanamume mmoja kwa Jina John ndiye  aliyemwajiri ili ambebee mzigo huo ila Mahakama ya Vietinamu ilisususia kuitikia ombi na rai za Bi Nduta na badala yake koti ikaamuru anyongwe.

Taifa la Vietnamu huweza kusawazisha wale wote ambao ni Rai wa taifa hilo au wageni kwa kuwanyonga pasi kuweka mipaka,katika miaka ya hivi Karibuni raia wengi wameweza kunyongwa, hivo kesi ya bi Nduta ni baadhi ya Kesi ambazo ziko huko vietnamu.

Hapa Kenya familai ya Bi Nduta iliweza kuomba taifa la Kenya kuingilia kati kumwauni mwanao dhidi ya Kunyongwa .

Seneta wa Kisii aliweza kuiomba serikali  ya Kenya kupitia kwa ubalozi wake Vietinamu Kuingilia kati  ili kumuani bi Nduta au akitumikie kifungu chake hapa Kenya.

Wito kutoka kwa umma na Diplomasia kwa Jumla, makundi mbalimbali yalirai Diplomasia ya Kenya kuingilia kati  kubaini chanzo kikuu ni nini kilikusudiwa kuwa raia wengi wanaopatikana huko ambao kipato chao ni haba huweza kunyanyashwa na mabwenyenye na kupagazwa na kuzingiziwa dawa za kulevya.