Wizara ya Ulinzi yakanusha taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya Sunday Nation na Taifa leo kuwa Raila Odinga aliokoa Rais Ruto kutoka nchi kuchukuliwa na Jeshi kufuatia maaandamano ya vijana wa Gen -Z Ya kupinga msuada wa Fedha wa 2024-2025.
‘’ Wizara ya Ulinzi ingependa kukanusha na kusema kuwa taarifa zilizochapishwa katika magazeti ya vyombo vya Habari ya Sunday Nation na Taifa Leo mtawalia yaliyokuwa na Mada nikinukuu RAILA: ‘’I saved Ruto from Millitary Coup’’ na Gazeti la Taifa Jumapili lenye mada ‘’Nilivyozima Mapinduzi Dhidi ya Ruto’’.
Barua hio ilioeleza kuwa machapisho hayo katika magazeti ya taifa hayakueleza na kufafanua vyanzo maalum vya madai hayo kuwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Zamani Raila Odinga katika mahojiano yake na vyombo vya kuwa alizuia uongozi wa Rais Ruto dhidi ya kuchukuliwa na Majeshi.
Wizara ya ulinzi wa taifa la Kenya ilitaja Habari hizo kama za uongo,hazina msingi,zizizokuwa na Mashiko ,Habari za Kupotosha na za kimzaha .
Kupitia kwa barua hiyo ujumbe ulizidi kueleza kuwa Wizara ya ulinzi ni taasisi ambayo ina maadili na ambayo ilijitolea kufanya kazi kwa heshima ,maadili na kutumikia taifa kwa haki,usawa na uwazi.
Jeshi la taifa litasalia kuwa imara na tiifu kwa Rais ambaye ni amri jeshi mkuu wa majeshi yote ya taifa na liko imaara na tayari kwa kulinda taifa kwa hali na mali pasi kuegemea mirengo ya kisiasa au kuwa na masilahi ya binafsi.
Machapisho ya Taifa Leo na the Sunday Nation yalitoa taarifa zisizo za kweli na ambazo vyanzo vyake havithaminiki ifaavyo na lengo la machapisho hayo yalikiuka uzalendo wa nchi na kujikita katika lengo la kuongeza idadi ya wasomaji huku yakikwepa ustaarabu wa wanahabari inavyostahiki.
Hivyo wizara ya ulinzi ilitoa wito kwa mashirika ya vyombo vya Habari kuzingatia ukweli na maadili na vilevile usalama wa taifa haswa wanaporipoti masuala kuhusu usalama wa taifa barua ilifafanua kwa undani zaidi.
Wizara ya ulinzi inatoa taarifa ya kukanusha madai haya siku moja baada ya magazeti hayo kuchapishwa ambapo mhusika mkuu bwana Raila Odinga alihojiwa siku ya Jumamosi katika mahojiano yalifanyika nyumbani kwake Karen.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!