Mkuu wa Kitengo cha Mazingira katika Kaunti ya Nairobi bwana Geoffrey Mosiria alielezea sababu kuu ambayo uhasama kati yake na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ulipoanzia.
Alipokuwa akihojiwa na kituo Kimoja nchini Bwana Mosiraa aliweza kufafanua kuwa tofauti zao zilianza pale walipokuwa katika chuo kikuu cha Nairobi .
Alifafanua kuwa Mheshimiwa Babu kwa mara si moja ameishi kwa misemo kuwa hamna siku ambayo atawahi kuja kushindwa au kuwa mtu kando na kuwanianafasi ya kiti cha uongozi katika chuo kikuu.
Bwana Mosira aliendelea na kusema kuwa alishindana na babu Owino lakini aliibiwa Kura katika chuo kikuu cha Nairobi.
‘’Uhasama wangu na Babu ulitoka mbali ,Babu huwa anaamini kuwa mimi sitawahi mshinda kwa vyovyote vile kando tu na kuwania siasa za vyuoni ama sitawahi Kuwa chochote, Nilishindana na Babu katika kura za kusaka uongozi chuo cha Naoirobi.
Kutokana na Babu kuwa alikuwa amejulikana na uongozi wa chuo sana aliweza kuibiwa kura na na kutangazwa mshindi aidha mkuu wa Kaunti ambaye amepata umaarua mwingi katika Mitandao ya Kijamii kutokana na hatua yake ya kusuluhisha majanga yanayotokana na Mazingira .
Alifafanua akisema kuwa alisema kuwa Babu alimtafuta kumwarifu kuwa alikuwa na azma ya kuwania kiti katika eneobunge la Embakasi Mashariki mwaka wa 2017.
Kulingana na Mosira chama cha ODM kilimtaka asimame ili aweze kutwaa ushindi wa chama hicho Alisema kuwa katika uchaguzi uliofuata vilevile alimtafuta ambapo waliketi katika mkahawa mmoja sehemu za Kileleswa ili kuzungumzia masuala ya siasa.
‘’Bwana Owino alinirai kwa sababu mimi ni binadamu nilimuelewa na kumpa kibali cha kuendelea’’ Bwana Mosira aliendelea kufafanua kuwa huwa anamwogopa akidhani kuwa huwa anadhani kuwa anapana kuwa mpinzni wake mkuu katika kinyan’ganyiro cha kusaka uongozi wa eneo bunge la Embakasi Mashariki.
Bwana Mosira alionekana kumushauri Babu Kutekeleza wajibu wake kama mbunge kwa kuhakisha kuwa anawapa wananchi waliomchagua maendeleo ya kudumu na badala yake aache kuingilia kazi za huduma za usafi wa Kaunti kwa kutuma takataka katika mitandao malimbali ya kijamii kuashiria kuwa kazi haifanywi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!