
NI mwaka mmoja sasa umepita tangu kifo cha ghafla cha aliyekuwa TikToker mashuhuri humu nchini Brian Chira, shukrani kwa vimbwanga vyake vilivyowakera na kuwapunga wengi kwa viwango sawa.
Baadhi ya waliokuwa marafiki zake wa karibu wakiongozwa na Obidan Dela waliandaa hafla ndogo ya kumkumbuka Chira nyumbani kwao.
Dela kupitia ukurasa wake wa TikTok alichapisha video na picha akijumuika na baadhi ya wanafamilia wa Brian Chira nyumbani kwao huku wakikariri baadhi ya semi alizopenda kuzitamka mara kwa mara.
Katika video hiyo, Obidan Dela na Watoto hao walikuwa wameishikilia picha kubwa ya Brian Chira huku wakikumbuka na kukariri kauli aliyopenda kuitamka ‘kama wewe si pesa huwezi nipa stress’.
Pia waliimba kwa huzuni wimbo wa Otile Brown ‘One Call’ ambao ulisheheni sana wakati wa mazishi ya Chira ambapo ilisemekana ulikuwa moja ya nyimbo alizozipenda pakubwa.
“Yo guys, Obidan Dela hapa, guys, na niko na Brian Chira na Sophie Njeri Chira Kadogo na wananiambia kama vile Chira alikuwa anawaambia, ‘Kama wewe si pesa, huwezi ni-stress.’”
Nyota huyo wa zamani wa TikTok alikumbana na kifo chake baada ya kugongwa na gari usiku wa Machi 16, 2024 wakati wa msongamano wa barabarani alipokuwa akijaribu kuvuka kuelekea upande mwingine.
Dereva wa gari hilo alikimbia eneo la tukio, na mwili wake uligunduliwa kando ya barabara mapema asubuhi iliyofuata.
Kufikia wakati anaaga dunia, Chira alikuwa amekuwa gumzo kwenye programu maarufu ya kushiriki video, akiwa tayari amevuka idadi ya wafuasi 400,000.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!