Aiskrimu za koni

MTOTO mvulana mwenye umri wa miaka minne ameshangaza polisi baada ya kuwapigia simu akimshtaki mamake kisa alirudi kutoka shule akapata mama amekula ice cream yake.

Tukio hili la kushangaza na kufurahisha kwa viwango sawa liliripotiwa na shirika la Habari la Fox kwamba lilitokea siku chache zilizopita katika jimbo la Wisconsin, nchini Marekani.

Mnamo Machi 4, polisi walisema mtoto huyo aliwaelekeza nyumbani kwao ambapo alipiga simu kwenye 911 na kusema "mama yake alikuwa mbaya na alihitaji kwenda jela" kisha akakata simu.

Walipofika, mvulana huyo aliwaambia maafisa wawili aliowaita mamlaka baada ya mama yake kula aiskrimu yake na kwamba huenda jela lilikuwa chaguo pekee.

Kisha akabadili mawazo yake na kusema "hakutaka tena aende jela na alitaka tu ice cream," polisi walisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika picha za kamera zilizovaliwa na polisi, zinazoonekana juu ya hadithi, maafisa wanasikika wakimueleza mvulana huyo, "Hakuna kupiga 911 isipokuwa ikiwa ni dharura halisi, sawa?"

Kwenye video hiyo, mama yake alisema hii ilikuwa "mara ya kwanza kufanya kitu kama hiki," akielezea, "Jinsi alivyofanya ilivutia sana. Alipiga simu na akamwambia Siri, akasema, 'Halo, Siri. Piga polisi. Mama yangu ana tabia mbaya.'”

Maafisa hao walijitokeza siku iliyofuata wakiwa na aiskrimu kwa mtoto huyo wa miaka 4.