LILLIAN nganga

ALIYEKUWA mke wa msanii Juliani, Lillian Nganga amewaziba midomo wale ambao wamekuwa wakimtupia maneno ya kila aina, siku chache tu baada ya kuweka wazi kwamba penzi lake na rapa huyo wa ‘Utawala’ lilizama.

Kupitia ukurasa wake wa X mnamo Machi 12, Nganga alisema kwamba haoni sababu yoyote kwa watu kumrejelea kama mjinga mitandaoni kisha kuvunjika kwa mahusiano yake ya kimapenzi.

Kwa mujibu wake, yeye haoni aibu yoyote kuvunjika kwa mahusiano yake ya kimapenzi kwani amekuwa na wanaume wawili tu tangu alipokuwa na umri wa miaka 25 hadi sasa anapoelekea miaka 40.

“Je, ukweli kwamba nimekuwa na wanaume wawili tu tangu nikiwa na umri wa miaka 25 (ninatimiza miaka 40 mwaka huu) unawezaje kunifanya mambo yote ya kipuuzi mnayoniita? ? Pumbavu, Wajinga sana!” Lillian Nganga alichapisha.

Akirejelea uhusiano wa zaidi ya miaka 10 na aliyekuwa gavana wa Machakos ambaye sasa ni Waziri wa leba Alfred Mutua ambao ulivunjika mwaka 2021, Nganga alisema kwamba anajionea Fahari kuwa miongoni mwa watu waliosimama na mwanasiasa huyo katika kampeni mara mbili na kushinda ugavana naye.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Nganga aliyeonekana kusimama kidete pasi na kutetereka dhidi ya mashambulizi kutoka kwa wanamitandao alisema kwamba huo ni mwanzo tu na yeyote ambaye atashindwa kustahimili majibu yake basi ajiondoe mapema kwenye gumzo.

“Nilikuwa na bahati ya kuendesha chaguzi mbili na kushinda (jambo ambalo baadhi yenu hamtawahi kupata uzoefu), kwa hivyo upende usipende, nitaendelea kushiriki maoni yangu kuhusu mambo tofauti. Huu ni mwanzo tu. Chafua kubaki au kujiondoa,” alisema.

Chapisho la Lillian Nganga

Katika mahojiano ya kipekee na Dr Ofweneke, mke wa gavana wa zamani wa Machakos na mwandishi alizungumza kwa uwazi kuhusu mtazamo wake kuhusu mahusiano, akiweka wazi kuwa haamini kushikilia wakati kitu kimeenda mkondo wake.

Alisema kwamba anapendelea kukumbatia uzoefu, kuthamini masomo aliyojifunza, na kusonga mbele bila mapambano yasiyo ya lazima.

"Sitatizika kushikilia tu kitu wakati wakati wake umekwisha. Ninathamini kile tumekuwa nacho, kumbukumbu au masomo, kisha tunaendelea tu,” Lillian alishiriki, na hivyo kuonyesha kwamba hakuwa na majuto kuhusu mahusiano yake ya zamani.