Gidi na Ghost

ONGUSH Ongura, mwanamume kutoka kaunti ya Busia ni mwanamume mwenye msongo wa Mawazo baada ya kukosana na mkewe.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32 alipeleka mahangaiko yake kwenye kitengo cha Patanisho kwa Gidi na Ghost kwenye Radio Jambo akiomba kupatanishwa na mkewe.

Kwa mujibu wa Ongura, walikosana na mkewe, Naliaka Simiyu mwenye umri wa miaka 28 baada ya kuenda Saudi Arabia na kurudi bila kurudi katika ndoa yake.

“Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka tatu na tuko na Mtoto moja. Nilikosana na Bibi yangu mwaka wa 2022 baada ya mimi kukubali aende Saudi Arabia for 2yrs na alirudi May 2024. Baaya ya yeye kurudi hata hakufika nyumbani kwangu hata kwao pia. Akisikia sauti yangu kwenye simu anakata, mimi naomba nijue msimamo wake tu,” Ongura alieleza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Alieleza kwamba walitoka nyumbani kuja Nairobi ambapo mkewe alipata nafasi ya kuenda Saudia na hadi ikaidi wakakubaliana kutoa mimba ambayo alikuwa nayo ilia pate kusafiri.

“Nilikuwa na mke nyumbani nikakuja Nairobi na yeye na tukaelewana akatoa mimba ili aende Saudi Arabia. Akafika huko baada ya mwaka akanitumia pesa 40k nikajenge nyumba. Nikamwambia siwezi jenga mpaka akuwe karibu akakasirika akaniblock. Hiyo pesa nikaongeza zingine nikanunua pikipiki. Sasa aliporudi hakufika kwangu na kwao hajaonekana,” Ongura alisema.

Alithibitisha kwamba mtoto ako na yeye na mkewe hajawahi fuatilia kuhusu maendeleo ya malezo ya mtoto wao.

Gidi na Ghost walipompigia Naliaka simu, alieleza kwamba hakuna cha kuelewana na mumewe.

Naliaka alieleza kwamba mumewe alimuonyesha madharau baada ya kumtumia pesa kisha akazima simu, na kusisitiza kwamba hii haikuwa mara ya kwanza bali ni mazoea ya Ongura.

“Huyo ni jamaa ambaye hasaidiki na hakusaidii pia,” Naliaka alisema.

Hata hivyo, mwanamume huyo alikubali makosa hayo na kusingizia ujana lakini akamuomba Naliaka kurudi kwa ajili ya kulea mtoto na kusema kwamba kwa sasa ameshakua kiakili.

Ni ombi ambalo Naliaka alikataa katakata kurudiana na yeye huku pia akidinda hata kutaka kumuona mwanawe.

“Nilikuachia mtoto ndio usinifuate eti nilienda na mtoto wako. Sitaki!” Naliaka alimwambia Ongura.

Naliaka alimaliza kwa kumfichulia Ongura ukweli kwamba kwa sasa ameshaoleka kwingine na tayari ako na mimba.