
RAIS William Ruto ameonekana kuvutiwa na jinsi Wakenya wamekuwa wakibuni majina ya kumrejelea na kusema kwamba haoni ubaya katika majina hayo
Akizungumza katika siku yake ya 3 kwenye ziara ya wiki moja kwenye kaunti ya Nairobi huko maeneo bunge ya Kibera na Lang’ata Alhamisi, Ruto alisema kwamba Wakenya hawajaanza sasa kumbandika majina hayo.
Kiongozi huyo ambaye alionekana kuwa mwingi wa furaha aliwaambia Wakenya kwamba watamuua kwa majina, akichukua fursa hiyo kuimba kionjo cha wimbo wa ‘Kasongo’ – moja ya jina ambalo amebandikwa.
“Wacha niwaulize nyinyi Nairobi, Langata... si nyinyi mtaniua na majina?” Rais aliuliza kwa utani.
Kiongozi huyo wa nchi alitaja baadhi ya majina ambayo amekuwa akibandikwa na Wakenya, si tu baada ya kuwa rais bali pia huko nyuma hata kabla ya kuwa rais.
“Sasa mimi nataka niwaulize, mlianza huko mkasema Hustler, halafu mkasema Survivor, kisha mkaenda jina lingine, Zakayo. Sasa nimesikia mmeongeza lingine, Kasongo. Sasa haya majina mtaongeza hadi yafike mangapi? Eeh? Bado mtaongeza lingine ama hayo yametosha? Haki nyinyi mko na maneno. Sasa nyinyi mnataka haya majina yangu yafike mangapi?”
“Mnataka yafike 10? Sasa nitaongeza William Kipchirchir Samoei Ruto Hustler Survivor Zakayo Kasongo...sijui nani. Anyway, ni sawa tu. Tuendelee. Ama mnasemaje bwana?” rais Ruto alitania.
Baadae katika eneo la Toi, rais Ruto aliwapakulia wanafunzi msosi wa Chapati na kutaarifiwa kwamba tayari Wakenya wamebuni jina lingine kumrejelea kama ‘El Chapo’ – jina ambalo alisema nis awa kwake pia.
“Hata hiyo ya chapo pia nis awa,” rais Ruto alisema huku akiwapakulia wanafunzi chapati.
Rais amekuwa akizuru maeneo na kuzindua miradi mbalimbali katika kaunti pana ya Nairobi tangu Jumatatu wiki hii.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!