Mwakilishi wa kike wa Nairobi Bi Easther Passaris na mheshimiwa ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya siasa Bi Juliah Chege kwa Pamoja waliwarai vijana kuwa watulivu na kutokubali kugawanywa kwa misingi ya Kikabila na wanasiasa walio na maslahi ya binafsi.
Viongozi hao wakihojiwa katika kituo kimoja cha humu nchini walidadavua wazi kuwa kuna hulka potovu miongoni kwa vijana ambayo imepandwa na baadhi ya viongozi wanasiasa ili kuleta hali ya sintofahamu nchini.
Easther Passaris katika usemi wake aliweza kueleza kuwa ipo haja ya kulea jamii iliyo na maadili kwanzia nyumbani ,kanisani ,shuleni ,vyuoni hadi katika viwango vya kuitwa wazazi wa siku za usoni.
Aliweza kusema kuwa serikali ilikuwa ikijitahidi kwa ajili ya kuwatengenezea vijana ajira ambayo itawasaidia kukimu maisha ya siku zao za usoni na kuwataka vijana waweze kuwa na mitazamo Chanya katika kazi na kwa viongozi wao.
‘’Sasa hivi serikali inaendeleza mpango wa kuzindua vyanzo vya kusomea masuala na teknologia kote nchini alimaaru ‘’computer hubs’’ kwa hivyo ninarai vijana kuchukua fursa hio kupata elimu ya mitandaoni badala ya kushinda kila wakati wakilalama na kupiga kelele’’ Passaris alisema.
Aliweza kufafanua kuwa ipo miradi mbalimbali ambayo serikali inajitahidi ili kuhakikisha kuwa maisha ya vijana wetu inakuwa katika mkondo mzuri kama vile kuwa na ajira ya kazi mtaaani ,ila akasema kuwa wapo baadhi ya watu wengine wanaokosoa mpango huo kwa kuwachochea watu kutofanya ilihali wao wana ajira.
Alisisitiza kuwa umoja na mshikamano wa nchi hupatikana ikiwa kuna amani na utulivu ,iwapo viongozi wanashirikiana hiyo ni ishara kuwa kutakuwa na maendeleo kila pembe ya nchi pasi kubaguliwa
Kwa upande wake bi Chege naye alirai vijana kutokubali kuingizwa katika siasa za migawanyiko huku akiwaomba vijana kuwa imara kutetea maslahi yao kwa kutumia njia za kisheria pasi kuzua fujo wala kuchanganywa na viongozi ambao azma yao ni kutaka kuwagawanya vijana kwa misingi ya kikabila na kuchochea ghasia .
Hata hivyo Bi Chege aliweza kutoa wito kwa serikali kufanya hima ili kuwapa nafasi za ajira vijana au nafasi mbalimbali ili kuepuka hilo joto la kisiasa ambalo linazidi kupanda huku vijana wakikemea viongozi wa serikali kila uchao na kuwabandika majina ambayo si mazuri wito sawia na huo uliweza kutolewa na Profesa Fred Ogola ambaye ni kaimu mhadhiri mkuu chuo cha Strathmore.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!