Aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua Kiongozi wa Wiper bwana Stephine Kalonzo Musyoka na baadhi ya Wakenya wengi walionekana kutoa hisia na maoni tofauti kuhusu michango ya Rais William Ruto Makanisani.

Rais Ruto kwa siku kadhaa zilizopita  alionekana kutoa michango ya mamilioni katika makanisa mbalimbali kama njia mojawapo ya kuonyesha ushirikiano baina ya serikali na dini.

Juhudi hizi zinapoendelezwa na Rais kwa kutoa michango ya Harambe katika makanisa mbalimbali aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gathagua, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka,  baadhi ya Wakenya na viongozi wa dini kutoka sehemu tofauti za nchi walionekana kupinga mikakati hiyo ya Rais ya kuchangisha mamilioni walikosoa mpango huo wakiutaja kama kejeli na madharau na wengi wakisawiri kitendo hicho kama kicheko kwa Wakenya.

Mnamo Novemba 19,2024 katika kanisa la Katoliki  la Soweto Kayole Rais alipohudhuria ibaada na waumini wa dhehebu hilo  aliweza kutoa mchango wa kitita cha shilingi milioni mbili na laki sita 2.6m kwa ajili ya kujengea mchungaji nyumba na kukamilisha ujenzi wa Kanisa.

Keshowe baada ya kanisa hilo kupokea mchango huo kutoka kwa kiongozi wa taifa, Askofu  Philip Anyolo anayesimamai jimbo la Nairobi katika taarifa yake alisema kuwa  walipokea sadaka ya mchango huo ila  viongozi hawakueleza uhalisia wa  michango hio hivyo  ilikosa maadili basi hawakuwa na budi bali kurudisha mchango huo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika maelezo yao yaliosababisha kurudisha kwa hela hizo taarifa ya Pamoja kulingana na mjibu wa Askofu Anyolo alikariri kwa kusema kuwa kanisa liko huru na wazi kupokea matoleo na sadaka ambayo ni takatifu na ambayo vyanzo vyake si vya kutiliwa shaka hivo maadili ni nguzo muhimu katika kila mchango,  michango ya aina hiyo ilikiuka mswada wa kutoa michango wa mwaka wa 2024.

Mnamo Machi 3,2025 katika kanisa la Jesus Winners Ministry linaloongozwa na Mhubiri Mwai kutoka Roysambu Rais alipohudhuria ibaada katika kanisa hilo aliweza kutoa mchango wa shilingi milioni ishirini 20m na kuahidi kutoa mchango mwingine katika Harambe wa shilingi milioni mia moja kwa ajili ya ujenzi wa kanisa.

Isitoshe Jumapili ya Tarehe 9, Machi 2025 katika kanisa la AIC Fellowship  Annex Eldoret Rais alipohudhuria ibaada aliweza kutoa mchango wa shilingi milioni ishirini 20m na kuahidi kuendelea kutoa michango na kushiriki katika Harambe mbalimbali za kuchangiza pesa.

Kutokana na huu msururu wa Rais kushiriki katika michango mbalimbali viongozi mbalimbali Pamoja na Wakenya wengi wametilia shaka uhalali wa  pesa hizo wakihitaji uchunguzi wa dharura kuanzishwa ili kubaini au kuweka wazi pale ambapo hela hizo hutoka ikikusudiwa kuwa hali ya Uchumi na biashara ni mbaya kwa wakenya wengi.

Maoni tofauti kutoka kwa Wakenya walitoa wito kwa Rais wakimrai aelekeze michango hiyo pia kwa wakenya walalahoi na kuwapa nafasi ya kujiunua vilevile walisema pesa hizo zilifa kuelekezwa kwa Bima ya matibabu ya SHA ili kutatau zogo la kutofanya kazi kwa kuwatibu wagonjwa hospitalini.