Maafisa wa polisi kutoka nchi ya Ufilipino walimkamata rais wa zamani Rodrigo Durtete baada ya mahakama ya jinai ya ICC kutoa amri ya kumkamata kwa tuhuma za kuwaua binadamu wengi kuhusu vita dhidi ya mihadarati.
Durtete ambaye ana umri wa miaka 79 alifikishwa kizimbani muda mfupi tu baada ya kutua kutoka kwa ndege katika uwanja wa Manila kutoka Hong Kong China.
Rais huyo wa Zamani hakuomba msamaha kwa kutekeleza kitendo cha unyama kwa kuwaua maelifu ya raia katika msako wa vita dhidi ya dawa za kulevya alipokuwa rais mwaka 2016 hadi 2022.
Alipokuwa akishikwa aliweza kulalama kwa kusema kuwa hakuna hatia yoyote aliyokuwa ametekeleza,aliyekuwa msemaji wake wa zamani Salvador Panelo alilaani kukamatwa kwake akiutaja kama kinyume cha sheria akisema kuwa Ufilipino ilikuwa imejiondoa katika mahakama ya ICC mwaka 2019.
Mahakama ya ICC ilikuwa imetoa tangazo kuwa ilikuwa na haki za kisheria kuiwadhibisha Ufilipino hata kabla ya kujiondoa katika mahakama hiyo .
Hata hivyo wanaharakati walisifia kukamatwa kwa Durtete na kuutaja kama historia kwa kuwanyanyasa na kuwaua watu Kinyama jambo ambalo lilisifiwa na muungano wa makundi ya kutetea haki za binadamu ( ICHRP).
Bwana Durtete alikuwa Hong Kong akifanya Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Mei 12 wa kumchagua Meya wa jimbo la Davao.
Video zilizonaswa na kuonyeshwa katika runinga moja zilimuonyesha bwana Durtete akitembea akiwa amebeba ubati huku taarifa zikisema kuwa yuko salama na yuko chini ya uangalizi wa madaktari wa taifa.
‘’Dhambi yangu ni nini nilifanya jukumu langu vyema kama rais la kuhakikisha kuwa kuna amani kwa wafilipino na kwa taifa zima kwa jumla’’ Durtete alisema.
Alikuwa akiwahutubia wafuasi wake waliokuwa wakimshangilia kwa mbwembwe kabla ya kuondoka Hong Kong.
Durtete alihudumu kama Meya wa Jimbo la Davao kwa zaidi ya miaka 22 na alilihakikishia taifa lake usalama wa kiwango cha juu katika vichorochoro mbalimbali.
Katika enzi zake aliweza kuhakikisha kuwa amani imetawala na kuonekana kama kiongozi mwenye msimamo mkali ambapo aliweza kuwapiku wapinzani wake katika uchaguzi wa 2016 uliokuwa na ushindani mkali.
Katika utawala wake aliweza kuamrisha vikosi vya usalama kuwapiga na kuwaua raia waliojihusisha na ulanguzi wa dawa za kulevya zaidi ya watu 6000 walipigwa kwa mitutu ya Bunduki na kuuawa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!