
Afisi ya mdhibiti wa bajeti za umma bi Margaret Nyakang'o ilitoa ripoti ya kusema kuwa Kaunti nyingi zina madeni mengi ambayo hazijalipa.
Kulingana na ripoti ya mwaka wa 2025 amabyo ilielezea hatua ambazo Kaunti zilipiga katika kuzalisha pato lake na kuimarisha viwango vyake vya fedha.
Mdhibiti wa bajeti za umma aliweza kurodhesha baadhi ya sababu kadhaa ambazo huweza kufanya Kaunti kutotumia hela zake ipasavyo kwa mfano Kaunti kutenga bajeti ya hela nyingi hatimaye inashindwa kuziweka katika mikakati ya matumizi ipasavyo.
Ripoti ya mdhibiti wa bajeti za serikali iliweza kusema kuwa Kaunti nyingi huweza kutumia na kutegemea fedha nyingi ambazo huwa zimetengewa wizara ya Afya kwa minajili ya kuhakikisha kuwa vifaa vya hospitali vinakuwa katika hali njema pesa hizo huishia kutumiwa kama mbadala kwa matumizi mengine.
Vilevile ripoti hiyo iliweza kudadavua kuwa mara nyingi Serikali za Kaunti huweza kupanga na kukadiria kiwango kikubwa cha pato la Kaunti Pamoja na pato kutoka kwa Serikali kuu jambo ambalo ikiwadia wakati wa kuanza kutekeleza matozo ili kukimu kiwango hicho cha bajeti huwa ni vigumu sana.
Ripoti ya mdhibiti wa bajeti ya serikali iliweza kueleza kwa upana kuwa kuna matumizi mengine ya pesa za Kaunti ambazo huwa hayabadiliki licha ya kuwepo kwa mifumko wa bei za bidhaa
Ripoti ya mkaguzi wa bajeti za serikali vilevile iliweza kusema kuwa mara nyingi serikali za Kaunti huweza kutumia hela nyingi kwa masuala ya burudani na usafiri wa safari za nje ambazo huhitaji kutengewa bajeti yake ambayo huweza kufyonza Magatuzi pesa nyingi sana.
Kulingana na maoni yake Seneta wa Kisii Richard Onyoka alisema kuwa Kaunti nyingi zinakumbwa na hali tata ya kuthibiti hali na mifumo yake kifedha ni kwa sababu ya kukuwa na viongozi ambao hawataki kuwajibika ipasavyo na vilevile kukosa hali ya uchanya na uwazi katika kupokezana mamalaka.
Seneta alielezea akisema kuwa mara nyingi utawala unaondoka mamlakani huweza kuwacha madeni mengi kutoka kwa kampuni zilizokuwa zikisambaza bidhaa kwa muda wa kipindi cha miaka mitano huku deni hilo likikuwa kubwa na hivyo basi kwa Bahati mbaya utawala mwingine unapochukua hatamu za uongozi huweza kutupilia mbali madeni ya awali na kuanza upya.
Ripoti za aina hii zinapoifikia afisi ya mdhibiti wa hesabu za serikali huweza kususia kuandika ripoti ya kuidhinisha malipo ya hela kwa Kampuni husika hivyo kufanya Kaunti kuwa na madeni makubwa na vilevile kuanza kukopa pesa kwa benki na kwa hazina za serikali kuu bila mipangilio na utaratibu maalimu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!