
MWANAMITINDO Amber Ray ametoa maoni yake kuhusu watu ambao wanafanikiwa maishani.
Kulingana naye, anahisi kabisa wakati mwingi mtu ambaye ni mwaminifu sana haipati njia ya mafanikio, akidokeza kwamba wakati mwingine ufanisi upo katika ukiukaji wa baadhi ya sheria.
Ray alitoa maoni haya kupitia ukurasa wake wa Instagram akisema kwamba anahisi kaisa mtu yeyote aliyefanikiwa maishani, hakufuata sheria na masharti yote bali kuna moja au mawili ambayo alikiuka ili kuyafikia mafanikio yake.
“Sijui ni nani anastahili kusikilia hili lakini nahisi dunia haijaundwa kwa ajili ya mtu mwaminifu kufanikiwa. Wakati mwingine sheria sharti zivunjwe ili mtu kupata ufanisi,” Amber Ray alsiema.
Mama huyo wa Watoto wawili anayejiita ‘bibi ya tajiri’ alisisitiza kwamba si kwa nia mbaya lakini watu wengi waaminifu wakati mwingi huishia kuumia kwa kutumiwa kwa njia isyofaa.
“Kama utafuata sheria zote kwa uzuri, huenda utajipata katika umaskini. Sauti ya mtu mwaminifu huwa imefinywa katika koo lake,” Amber Ray aliongeza.
Amber Ray aliibuka na maoni hayo, siku chache baada ya kuzua mzozano kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhalali wake kujiita bibi ya Tajiri.
Baadhi walihisi kwamba mtu anayestahili kujiita bibi ya Tajiri ni yule anayefanyiwa mambo makubwa na ya kipekee na mpenzi wake, wakitolea mfano wa Diana Marua ambaye mwezi uliopita alikabidhiwa zawadi 8 ghali na mumewe kusherehekea miaka 8 ya ndoa.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!