Vera Sidika

SOSHOLAITI Vera Sidika ametoa wito kwa mahoteli na migahawa kuwajali wateja wao haswa wanawake ambao wana umbile kubwa.

Kupitia kurasa zake kwenye Facebook na Instagram, Sidika alieleza mafadhaiko na mateso ambayo watu wenye viuno vipana kama yeye hupitia katika sehemu nyingi za starehe na burudani.

Alitoa ombi la kipekee kwa niaba ya wengine waliobarikiwa na mwili kama yeye akitaka wamiliki wa mahoteli, migahawa na sehemu zingine za starehe kutenga viti mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji na starehe zao.

Mama huyo wa watoto wawili alijitokeza kama mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye viuno vipana, akisema kwamba wengi wanateseka kwenye sehemu za burudani na maadamu hawasemi, basi yeye atakuwa msemaji wao.

‘Mahangaiko ambayo tunapitia huku nje sio mzaha. Jamani migahawa, tunahitaji viti vikubwa. Maisha ya wasichana wanene yana umuhimu pia,” Sidika aliandika.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Ikiwa hilo halitoshi, aliambatanisha malalamiko yake na video yake ya kuonyesha uhalisia jinsi yeye binafsi anateseka.

Sidika, ambaye katika video hiyo alionekana kwenye vazi la rangi nyekundu aliingia katika mgahawa mmoja na kufanya majaribio ya kuketi katika viti kadhaa lakini vyote vilionekana kumbana na kukera starehe yake.

Sidika si mwanamke mwenye umbile nene wa kwanza kulalamika kuhusu wembamba wa viti vya sehemu za starehe kubana starehe zao.

Novemba 2024, mshawishi wa masuala ya usafiri kwa jina Jaelynn Chaney alichukua kwenye TikTok kulalamikia mashirika ya ndege kuwatengea watu wanene viti vyao spesheli.

'Hii haihusu kuwapa watu wanene zaidi - ni kuhusu kukidhi mahitaji ya kimsingi.'

Influenza huyo wa usafiri wa ukubwa wa juu amehubiri kwa muda mrefu kuhusu hitaji la viti vikubwa kwenye ndege, huku akidai kampuni kuu za usafiri wa anga zinaendelea kupunguza viti na kusababisha msongamano wa abiria zaidi.

Kwa mujibu wake, vipimo vya viti vya sasa mara nyingi havifurahishi na wakati mwingine hata vinabagua abiria wakubwa, na kuwafanya kuhisi kulazimishwa kununua viti vya ziada au kukabiliwa na usumbufu wakati wa safari za ndege; suala hili mara nyingi huangaziwa na watetezi kwa kutumia maneno "usawa wa mwili katika usafiri.".