
MCHEKESHAJI na mtangazaji wa redioni, Dr Ofweneke amefafanua kwa nini mtu kujitambulisha kama mpenzi wako wa zamani kunafaa kuwa na mwisho.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ofweneke alisisitiza kwamba ipo haja ya muda kuwekwa wa mtu kujitambulisha kama mpenzi wako wa zamani, na muda huo ukiisha, nyinyi mnabaki tu kuwa watu mliowahi kukutana na wala si wapenzi wa zamani.
Akitolea mfano, Ofweneke alisema kwamba haiwezekani mtu kujitambulisha kama mpenzi wa zamani wa mtu Fulani hali ya kuwa mahusiano yao yalivunjika mwaka 2000 – zaidi ya miaka 25 iliyopita.
“Kuwa Ex wa mtu kunafaa kuwa na tarehe ya mwisho. Siwezi kuwa Ex wako na tuliachana mwaka 2000. Baada ya mwaka mmoja, unafaa kuniona kama mtu wa kawaida tu ambaye ulikutana naye,” Ofweneke alieleza.
Kauli hii ilivutia maoni kadhaa baadhi wakikubaliana naye huku wengine wakipinga kwamba moyo na akili havina uwezo wa kufuta na kusahau hisia za zamani hata iwe ni miaka mingapi imepita.
Waliokubaliana naye walidai kwamba mtu anafaa tu kusalia kuwa Ex wako ikiwa kuna ushahidi wa watoto kutokana na uhusiano wenu.
Haya hapa ni baadhi ya maoni;
@vivimusyoki: “Kama hakuna ushahidi wa watoto…sahau kuwa tuliwahi kukutana ??? hujambo mgeni.”
@lea.muthoni: “Mimi kama hatujazaa wewe sio ex wangu wewe ni kosa nililokutana nalo au mtu wa kubahatisha aliyeshirikisha mtu mzuri na mbaya.”
@lovely_nevin: “Truest.. our grandparents and our parents never talk of exes.. ??.. hii mambo ya ex ni kiherehere ya millennials kurudi chini.”
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!