
KANISA moja nchini Uganda limeripotiwa kuruka-ruka kwa furaha na vigelegele baada ya mwanasiasa wa upinzani kwa muda mrefu, Kizza Besigye kuripotiwa kuokoka akiwa kuizini.
Mwanasiasa huyo amekuwa kizuizini katika gereza la Luzira tangu Novemba 2024 baada ya kukamatwa Nairobi na kusafirishwa kinyemela ambapo anakabiliwa na shtaka la uhaini ambalo adhabu yake ni kifo.
Wachungaji hao ambao walionyesha furaha yao jijini Kampala Jumapili iliyopita walifurahia ripoti za kuokoka kwa Besigye wakisema kwamba hiyo ni kazi ya mikono ya Mungu.
"Hivi ndivyo Bwana anafanya…imeandikwa kwamba hakuna mtu anayeweza kuja kwa mwana isipokuwa baba amemvuta," alisema Mchungaji Fredrick Ssemazzi wa kanisa la Grace Assemblies Jumapili.
Taarifa za Besigye kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake ziliibuka kwenye vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita.
Mmoja kati ya wabunge wa zamani ambaye ni mwandani wa Besigye anayetambulika kwa jina Mubarak Munyagwa Sserunga alinukuliwa akieleza kuwa alithibitisha mwenyewe tukio hilo alipokwenda kumjulia hali Dk Besigye huko Luzira.
Dk Besigye, mgombea Urais mara nne amekuwa gerezani Novemba mwaka jana.
Anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kufuatia kukamatwa kwake na maafisa wa usalama wa Uganda nchini Kenya.
Awali, alikuwa amezuiliwa katika gereza la kijeshi na kupinga hatua hiyo kwa kususia chakula hadi kudhoofika kiafya kupelekea mamlaka kumkimbiza hospitalini.
Hata hivyo, Februari 23 mashtaka yake yalihamishiwa katika mahakama ya kiraia kama ambavyo mawakili wake walikuwa wanashinikiza.
Baada ya kusomewa mashtaka katika mahakama ya kiraia, Besigye alighairi mgomo wake dhidi ya mlo japo alizuiliwa tena.
Kesi yake inatarajiwa kuendelea leo hii Ijumaa ya Machi 7 katika mahakama hiyo, huku mawakili wake wakishinikiza kuachiliwa kwa dhamana.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!