
MCHUNGAJI wa kanisa la New Life Prayer Centre lililoko Mavueni kaunti ya Kilifi amejitokeza kimasomaso kutetea hatua ya rais William Ruto kutoa mchango wa shilingi milioni 20 katika kanisa moja kaunti ya Kiambu wiki jana.
Katika moja ya video za mahubiri yake ambayo imevutia hisia mseto ambapo alisema rais hujafanya lolote baya kutoa pesa hizo kwa ajili ya maendeleo ya kanisa.
Hii inajiri wakati ambapo rais Ruto amekuwa akikosolewa kwa kutoa mchanga wa shilingi milioni 20 katika kanisa la Jesus Winners Ministry wikendi iliyopita
Kwa mujibu wa Ezekiel, rais Ruto ni mtu mwenye pesa zake na hakukosea mtu yeyote kwa kutoa kiasi hicho kikubwa cha mchanga kanisani.
“Rais Ruto hana ndege? Helikopta si alikuwa anakampeni nazo? Huyu mtu atakuwa rais na hana pesa? Akitoa pesa zake aende akatoe sadaka, amekukosea? Acheni tabia mbaya nyinyi. Tuache hii tabia ya kukashifu kila kitu,” Ezekiel alisema huku akifichua kwamba alijua atazua gumzo baada ya kumkingia Ruto kifua.
Ezekiel aliendelea kumtetea Ruto dhidi ya dhana kwamba milioni 20 alizotoa kanisani ni za ufisadi, akisema kwamba mkuu wa nchi kando ya mshahara wa milioni 2, yeye ni mfanyibiashara mkubwa.
“Wewe unataka kuniambia rais Ruto hana pesa? Unataka kuniambia zile milioni 2 mnamlipa kama mshahara ndio pesa anategemea? Hapana… eti sasa akitoa 20m ni habari?”
Ezekiel alisema kwamba yeye amewahi fungwa na hii serikali – akirejelea masaibu yake miaka miwili iliyopita kutokana na matukio ya Shakahola – lakini akisema kwamba mahali ataona wananchi wanakosea sharti atawaambia.
“Hapo mnamkosea rais. Akitoa milioni 2 mnarudisha akitoa 5m mnarudisha na akitoa elfu 50 mtaanza kusema hiyo ni pesa gani rais mzima anatoa. Hapana. Kama mnachukia mtu mchukie yeye binafsi lakini msichukie urais,” Ezekiel alisisitiza.
Mchungaji huyo aliwarai waumini wake kutomchukia mtu ambaye anawapa chakula na kukitupa wakati hawana chakula chenyewe.
Licha ya kukosolewa vikali, rais Ruto pia amekuwa akipata watetezi ambao wamesimama kidete kutetea sadaka yake kanisani.
Kanisa katoliki limekuwa katika mstari wa mbele kumkosoa Ruto kwa pesa anazotoa kanisani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!