
RAPA matata wa humu nchini, Khaligraph Jones amewajibu baadhi ya watu wanaokosoa ngoma yake ya hivi majuzi, Khali Cartel 5 siku moja baada ya kuiachia.
Khali Cartel 5 ni mfululizo wa mkusanyiko wa rap zake ‘Cypher’ ambapo amekuwa akiwakutanisha pamoja wasanii kadhaa wa rap kumenyana kwenye ngoma moja ambayo huchukua zaidi ya dakika 10.
Khali Cartel 5 ambayo ameachia Alhamisi ina jumla ya dakika 12 na zaidi ya wasanii 5 wa rap.
Wimbo huo wa dakika 12, uliozinduliwa Alhamisi, Machi 6, 2025, unajumuisha safu ya wasanii wa kufoka wa Afrika Mashariki, wakiwemo Jakk Quill, Ruyonga, Fresh kama Uhh, Dyana Cods, Mex Cortez, na Abbas Kubaff.
Hata hivyo, baadhi walihisi kwamba haina ladha mpya kutoka kwa zile za awali nne na kumtaka kubadilisha mtindo na ladha kama anataka mashabiki waburudike na vitu vipya kutoka kwake.
“Mdundo ule ule wa zamani, mtindo ule ule wa kizamani, maneno yaleyale ya kizamani yanatumika tena katika kila pigo unalotoa. Sio kukuchukia kijana wangu lakini huu ni upuuzi,” shabiki mmoja kwa jina Bwire kwenye X alichapisha.
Khaligraph Jones, ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiwajibu mashabiki wake alimjibu huyo akimwambia kwamba katika mfululizo ujao, atakuwa anaimba kwa lugha tofauti.
Jones alijibu akisema kwamba ili kubadilisha ladha na mtindo, katika Khali Cartel ijayo atajaribu kuimba kwa lugha ya Kikisii.
Alimtaka mpishi maarufu ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa raga, Dennis Ombachi kuanza kumtayarishia mishororo ya kufokafoka nayo.
“Okay, the next one tutaimba na Ki kisii, @ombachi13 anza kubini verse #khalicartel5,” Khaligraph alijibu.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!