Mwenyekiti wa Bodi ya Udhibiti wa Kamari na Utoaji Leseni ya Kenya (BCLB), Dkt. Jane Mwikali Makau ametambuliwa kwa Tuzo ya kifahari ya Muungano wa Udhibiti, 2025 katika Kongamano la AGE mjini Lagos, Nigeria jukwaa kuu la kamari na udhibiti barani Afrika.
Tuzo hiyo inatambua juhudi zake za kuunganisha kanuni za michezo ya bahati nasibu kote barani Afrika, kukuza ushirikiano kati ya nchi na kudumisha viwango vya juu vya udhibiti.
Chini ya uongozi wa Mwikali, Kenya imekuwa kielelezo cha uchezaji wa kuwajibika, ikisisitiza uadilifu, utiifu, na mbinu bora za tasnia.
Utambuzi wa Dkt. Makau unaonyesha mchango wa BCLB katika kuanzisha sekta ya michezo ya bahati nasibu iliyopangwa na iliyodhibitiwa vyema barani Afrika.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki, ambaye sasa ni Naibu Rais, alimteua Jane Makau kuwa mwenyekiti wa Bodi ya udhibiti wa Kamari, na utoaji Leseni mwaka wa 2022 kwa kipindi cha miaka mitatu.
Yeye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati, na Ustawi wa Biashara na mwanachama wa Kamati ya Bodi ya Utawala na Ukaguzi (GRAC).
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!