siku ya wanawake duniani

MKUU wa Mkoa wa Arusha nchini Tanzania, Paul Makonda amewapa wanaume wote changamoto ya kuchapisha picha za wanawake wao kwenye mitandao yao ya kijamii kuelekea siku ya wanawake duniani.


Siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka itafanyika Jumamosi ya Machi 8.


Akizungumza na wanachi wake katika mkoa huo ulioko Kaskazini mwa Tanzania, Makonda alisema kwamba kila mwanamume anafaa kuingia katika challenge hiyo ya kupost picha ya mwanamke anayempenda.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


“Kuanzia kesho, kila mwanamume, kama kweli wewe ni mwanamume, na huyo mke uliye naye unampenda, kuanzia kesho tunaanza challenge wanaume kupost wake zao,” alisema.


Kamishna huyo alisema kwamba tayari yeye amemtaka babake kumpost pia mkewe – ambaye ni mamake.


“Kwa kuwa tarehe 8 ni siku ya wanawake, hiyo tunaiweka pembeni kuitumia kwa ajili ya wake zetu. Kwa mfano kama mimi nimemwambia babangu na yeye mapost mke wake. Mimi nitampost mke wangu. Kwa hiyo kuanzia kesho hebu tuone wanawake wanaopendwa na wanaume wao,” RC huyo alitoa changamoto.


RC huyo alitoa onyo kwa wanaume ambao wataibuka na visingizio kwamba hawako kwenye mitandao ya kijamii, akisema kwamba basi wampost hata kwenye WhatsApp.


“Sasa kuna watu wanasema ooh mimi sina Instagram, ooh sina Facebook’… mpost hata kwenye WhatsApp status. Yaani wewe kwenye Facebook humposti, kwenye Instagram humpost, kwenye DP ya profile humweki… aaah atakaa moyoni kweli huyo?” alihoji.


RC huyo alitetea changamoto hiyo kwa wanaume akisema kwamba licha ya kuisherehekea lakini pia ni njia moja ya kutaka kuona wanaume ambao wanawathamini wake zao.


“Kwa hiyo tunataka tusherehekee siku hii lakini pia tuone watu wanaojivunia wake zao kwa kuwa hakuna mafanikio yanayopatikana kama mwanamke hajashiriki kwa huyo mwanamume”


“Tutumie wiki hii pia kuwa kuwatia moyo wake zetu, kuwapa faraja na kuwatambulisha pia kwa jamii kwamba tunajivunia uwepo wao kwenye maisha yetu,” RC alirai wanaume.