
MMOJA kati ya wanawake kadhaa walioonekana katika video chafu kadhaa za jamaa kutoka taifa la Equitorial Guinea, Baltasar Engonga amejitokeza kuzungumzia athari ambazo kuvuja kwa video hizo kumemletea.
Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana, dunia nzima iliunganishwa pamoja na video chafu zilizodaiwa kuwa zaidi ya 400 ambazo Baltasar Engonga alidaiwa kufanya mapenzi na wanawake tofauti.
Mmoja wa wanawake walioonekana kwenye video hizo 400 za Baltasar Engonga amesikitika jinsi maisha yake yalivyobadilika sana tangu tukio hilo.
Katika video iliyovuma mtandaoni, alionekana akilia kwa uchungu huku akifichua kwamba hawezi kutoka nje ya nyumba yake tena kwa sababu ya kile ambacho watu wangesema.
"Siwezi kutoka tena baada yangu na video ya Baltasar kutokea," video hiyo ilinukuliwa.
Baltasar Ebang Engonga, mfanyikazi wa serikali katika Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Kifedha (ANIF), alikuwa gumzo katika mataifa mengi duniani baada ya kuvuja kwa video hizo.
Kulingana na ripoti, Engonga alirekodi kwa siri zaidi ya video 400 za maudhui chafu ambazo zinadaiwa kuwa na watu mashuhuri na wanafamilia wao, wakiwemo watu wa karibu sana na wasomi wa kisiasa wa Equatorial Guinea.
Inasemekana kuwa video hizi ni pamoja na wake, dada, na binamu za watu mashuhuri, na kufanya hii kuwa moja ya kashfa kubwa kukumba nchi katika kumbukumbu za hivi karibuni.
Kashfa hii ilitikisa duru za kisiasa za Equatorial Guinea, ambapo faragha na uaminifu vinathaminiwa sana.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!