
MBUNGE wa Embakasi Mashariki, Babu Owino ametoa ushauri kwa wanafunzi huku wanaporejea shuleni baada ya likizo fupi ya katikati mwa muhula wa kwanza.
Akizungumza bungeni wakati wanafunzi wa shule moja kutoka Embakasi walipozuru majengo ya bunge, Owino ambaye alipewa nafasi ya kutoa ushauri kwa wanafunzi hao na naibu spika Gladys Shollei aliwataka kutoendekeza mapenzi masomoni.
Owino alitumia lugha fiche kuwataka kuzingatia zaidi kalamu na vitabu vyao badala ya kukumbatia na kubusu wenzao wa jinsia tofauti shuleni.
“Kwa niaba ya mheshimiwa Mawathe, ningependa kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wanafunzi kutoka Eneobunge la Embakasi Kusini na ninataka kuwapa neno la ushauri kama watoto wetu,” Owino alisema.
“Elimu ndio njia pekee kuelekea mafanikio. Mizizi ya masomo ni michungu lakini matunda yake ni matamu. Wavulana kwa wasichana kumbuka ukiwa shuleni sasa hivi zingatia kwenye vitabu na kalamu.”
“Kama utambusu mwanamume, basi busu kitabu. Na kama utamkumbatia mwanamke basi kumbatia kalamu. Hicho ndicho kitu pekee ambacho kitakuokoa kutoka katika lindi la umaskini,” Owino aliongeza.
Video hiyo hiyo ambayo imevutia maoni mengi ya vichekesho ndio hii hapa chini;
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!