Burale aomba kutopigiwa kura

MCHUNGAJI Robert Burale ameshangaza sehemu ya wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukata uteuzi wake kuwania tuzo ya ‘Most Inspirational Man of God 2025’.


Burale alikuwa ameteuliwa kuwania tuzo hiyo na wababe wa injili kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika akiwemo Pastor T Mwangi lakini akaomba wafuasi wake kutofanya uthubutu wa kumpigia kura.


Kwa mujibu wake, ni fahari kubwa kutambuliwa Afrika na kuwekwa kwenye safu ya wanaostahili kuwania na kushinda lakini hahisi kama wito wake kueneza injili unafaa kuwekwa kwenye mizani ya kupigiwa kura.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


“Kwa jinsi ninavyothamini uteuzi huo, nawaomba wafuasi wangu kwa unyenyekevu wasinipigie kura katika kitengo hiki kwani siamini wito wa Mungu juu ya maisha yangu unapaswa kupigiwa kura,” Burale alisema.


Mtumishi wa Mungu alishukuru waandalizi wa tuzo hizo kwa kumteua lakini akisema hayuko tayari kushiriki katika kupigiwa kura, huku akifichua kwamba tayari alikuwa amewasiliana naye kuwaeleza kwamba amejiondoa rasmi hata kabla ya kura kupigwa.


“Kwa waandaaji asante kwa ishara lakini ninaondoa jina langu kwa unyenyekevu. MUNGU AWABARIKI. Ninahubiri tu kwa Neema ya Mungu ... kwa neema.”


“Nimewasiliana na waandaji rasmi lakini nimeweka hili hapa kwa sababu wafuasi wangu wengi wamenitumia ujumbe wakinihakikishia kura yao ...Kwa watu wote ninaowatia moyo huko nje Mungu apate utukufu,” Burale aliongoza.