Kennedy Rapudo na Amber Ray

MFANYIBIASHARA Kennedy Rapudo amewasifia wanawake kutoka jamii ya Akamba akisema kwamba ni kati ya jamii chache zinazotoa wanawake wanaojua umuhimu wa ndoa.

Rapudo alifichua hayo kupitia Instagram alipochapisha video ikimuonyesha mke wake, Amber Ray akimpakulia chakula kwa upendo.

Katika video hiyo, Amber Ray, ambaye anatoka katika jamii ya Akamba alionekana akimpakulia kinywaji moto mume wake huku akiwa amejawa na tabasamu ghaya.

Rapudo alifuatisha video hiyo na Kauli ya kuwasifia wanawake kutoka jamii hiyo, akisema jamii ya Akamba inatoa wanawake wazuri ambao wanajua kuhudumia wanaume wao.

“Wakamba ni watu wazuri sana. Unaona jinsi wanajua kuwahudumia na kutunza wanaume wao?” Rapudo alichapisha.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kauli yake inajiri wiki moja tu baada ya Amber Ray kuandikwa ujumbe wa kumshukuru mume wake kwa wapenzi baada ya kukamilisha mwisho wa mwezi wa mapenzi – Februari.

“Tunapouaga mwezi huu mzuri wa upendo, wacha tubebe joto na mapenzi yake katika kila siku inayokuja. Kumbuka, upendo hauzuiliwi kwa mwezi mmoja tu; ni safari endelevu inayoboresha maisha yetu kila siku.”

“Kwa mtu anayefanya moyo wangu kuimba, wewe ni mwamba wangu, msiri wangu, na furaha yangu kuu. Usaidizi wako usio na kikomo na upendo usio na kikomo hunitia moyo kila siku. Ninashukuru milele kwa nyakati tunazoshiriki na kumbukumbu tunazounda pamoja. Hapa ni kwetu, leo na daima,” Amber Ray alimvisha mumewe koja la maua.

Wawili hao wamekuwa katika huba la zaidi ya miaka 3 na pamoja wana mtoto mmoja binti, japo kila mmoja ana mtoto kutoka katika uhusiano wa awali.