Rayvanny

MSANII mmiliki wa lebo ya Next Level Music, Rayvanny amewaacha mashabiki wake na maswali mengi baada ya kuchapisha picha yake ya zamani kabla hajatoboa tundu kwenye tasnia ya muziki.

Msanii huyo ambaye amekuwa akisemwa kwamba ameshuka viwango kimuziki tangu aondoke katika lebo mama ya WCB mwaka 2022 amefuatisha picha hiyo na ujumbe wa kudai anapitia mambo mengi na magumu mno.

Hata hivyo, aliendelea kuonesha Imani huku akijipa moyo kwamba atashinda katika ujumbe huo aliojiandikia kama barua kwa nafsi yake.

“Mpendwa Rayvanny, ninakuonea fahari kubwa sana hadi hapo ulipofika. Ila nakuonea huruma sana, unapitia mengi sana ila usikate tamaa utashinda, nakuamini,” Rayvanny alijiandikia.

Ujumbe huo ulizua maswali na wasiwasi baadhi wakijaribu kung’amua kitendawili kilichoonekana Dhahiri katika ujumbe huo.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Wakati wengine walihisi huenda anazungumzia matatizo ya kimuziki, wengine walihisi ni matatizo ya kimapenzi, haswa baada ya kufichua mipango ya harusi yake mwezi Mei mwaka huu.

Haya hapa ni baadhi ya maoni ya watu;

@simba_wa_morogoro: “Sasa kama wewe mkubwa unapitia mengi, je machipukizi au wasanii wako itakuwaje?”

@msizwa23: “Usikate tamaa wewe ni bingwa ndugu yangu Rayvanny.”

@fobyofficial: “Utakuwa sawa, tenga muda wako zaidi wa kuongea na Mungu kwa sababu yeye ndiye mwenye sisis!”

@diddy_sepetu: “Nasubiri mwezi wa 5 tu hapa umuoe dada yetu.”