
BUNGE wa Mumias Mashariki, Peter Salasya ameonesha furaha yake baada ya ukurasa wake wa mitandao wa video fupi wa TikTok kufikisha wafuasi zaidi ya laki nane wikendi ilityopita.
Mbunge huyo anayejiweka kifua mbele kama mtetezi wa sera za vijana wa Gen Z alichukua kwenye ukurasa wake Facebook na kuwashukuru mashabiki wake 800k kwenye TikTok huku akisema kwamba Mungu ana sababu ya kumfanya yeye kuwa na ufuasi huo.
“Mimi sasa ndiye mwanasiasa anayeongoza katika kuwa na wafuasi wengi kwenye TikTok nchini Kenya. Kufikisha wafuasi 801400 kwenye tiktok na wewe ni mwanasiasa sio utani. Nataka kuwashukuru wakenya wote wanaofuata. Mungu ana sababu kwanini amenipa ufuasi huu mkubwa,” Salasya aliandika.
Aidha, mwanasiasa huyo kutoka chama cha DAP-K alisema kwamba atakuwa anatumia ufuasi huo mkubwa kama jukwaa la kutoa elimu ya kiraia kwa wakenya ili kuwasaidia katika kufanya maamuzi bora kisiasa.
“Jukumu langu sasa litakuwa kuwaelimisha wakenya elimu ya uraia na kuwafanya wafanye maamuzi sahihi katika uongozi na Utawala wa ardhi hii.”
Salasya ambaye wiki mbili zilizopita alinaswa akitiririsha moja kwa moja vikao vya bunge kwenye TikTok yake alitamba akisema kwamba anahisi hivi karibuni atakuwa kama chombo cha habari kutokana na ufuasi mkubwa anaozidi kupata kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii.
“Hivi karibuni nitakuwa media house kwa sababu ya ufuasi mkubwa wa wakenya. Endelea kufuatilia endelea kutoa maoni yako endelea kushare kile unachoona ni kizuri kwako,” Salasya alisema.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!