Chama cha ODM kinaadhamisha miaka 20 tangu kuasisiwa mwaka wa 2005 katika hafla inayohudhuriwa na vigogo wa chama hicho wakiongozwa Raila Odnga na katibu mkuu Edwin Sifun.
Ni Hafla ambayo imeratibiwa kufanyika Kaunti ya Busia katika shule ya Bukiri eneo bunge la Funyula .
Mkutano huo ambao utatarajiwa kuwaleta Pamoja viongozi,wanachama na wajumbe wote ili kuwa na mazungumzo ambayo yatalenga kuleta udhabiti chamani na muongozo mwema.
Mkutano wa sherehe hio unafanyika baada ya kinara wa chama hicho Raila Odinga kupoteza nafasi katika juhudi za kusaka wadhifa wa kuwa mwenyekiti wa AUC Afrika.
Kwa siku zilizopita Kinara huyo wa ODM amekuwa katika pilikapilika za kutafuta maoni ya mwelekeo wa chama kutoka kwa wananchi kote nchini.
Hata hivyo mkutano huo unapotarajiwa kufanyika kumekuwepo na hali ya kutoelewana kisera kati ya katibu mkuu wa chama bwana Sifuna na wanachama wengine chamani.
Itakumbukwa wazi kuwa ODM imekuwa na ukuruba wa karibu na serikali tawala ya Kenya Kwanza kwa kushirikiana kwa kile ambacho kilitwa serikali jumuishi(Broad Based Government).
ODM iliweza kutoa wanachama watano kujiunga na serikali ya Kenya kwanza Waziri Oparanya,Opiyo,Joho ,Mbadi na bi Doroth Oduor kutokana na hilo wengi wa wanachama wamekuwa wakiendeleza wito wa ODM kuunda mkataba wa ushirikiano na serikali.
Hata hivyo mkutano huo ukitarajiwa kufanyika Busia na Kuadhimisha miaka 20 tangu chama hicho kuanzishwa,katibu mkuu wa chama cha ODM bwana sifuna kwa siku za karibuni amekuwa mkosoaji mkuu wa sera za serikali huku akionekana kupinga misuada mbalimbali katika bunge la seneti.
Vilevile amekuwa akikosoa ushirikiano wa ODM na Serikali ya Kenya Kwanza akisema kuwa Serikali ya kenya Kwanza iliwafeli wananchi kwa kutotimiza ahadi zake jinsi ilivyoahidi katika manifesto yake.
Alipozungumza mnamo Ijumaa ya tarehe 28 Februari,2025 mjini Bungoma alipokuwa katika pilikapilika za kufungua ofisi za ODM, huko bwana Sifuna alizidi kutema madini ya uasi dhidi ya serikali ya Kenya Kwanza akiitaja kama serikali ambayo ilikosa dira imara ya kuongoza taifa.
Hata hivyo mkutano wa Busia unatarajiwa kutoa sura mpya na mwelekeo mpya ambao chama kitazingatia na kufuata iwapo tangazo rasmi litatolewa na kinara wa ODM bwana Odinga ambaye atatarajiwa kukabidhiwa mikoba ya uongozi tena baada ya kumtwika Profesa Anyang’i Nyong’o Gavana wa Kisumu.
Katika mkutano wa siku ya Ijumaa wa wajumbe wa ODM mwenyeji wa Kaunti hiyo ya Busia Daktari Paul Nyongesa Otuoma na mwakilishi wa kike Cathirine Omanyo ambao ni wanachama wa ODM ndio wenyeji wa hafla hiyo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!