Taasisi ya masomo ya matibabu ya KMTC kwa ushirikiano na KUCCPS zimetangaza nafasi 5000 kwa wanafunzi katika muhula na awamu ya mwezi wa tatu mwaka huu.
KUCCPS ilifungua mitambo yake mnamo Februari 26,2025 ili kuruhusu wanafunzi wenye nia kutaka kusomea kozi za utabibu waweze kutuma maombi.
Afisa mkuu mtendaji Daktari Kelly Oluoch aliwarai wanafunzi wote waliokuwa na azma ya kutaka kusomea taaluma hiyo kuchukua fursa hiyo kwa manufaa yao.
‘’Nafasi zipo kwa kwa kozi ishirini na moja (21) mtambo wa mtandao utasalia kuwa wazi kwa siku saba zijazo’’ Daktari Kelly alisema.
Daktari Kelly alisema kuwa wanaotuma maombi na ambao wanaomba na kuhitaji msaada wa kuelezewa zaidi kuhusu maombi yao au kozi wanaweza tembelea mabewa yao kwa usaidizi zaidi.
‘’Kwa kushirikiana na KUCCPS tumewaweka maafisa wetu katika mabewa yetu tofauti tofauti na kuwapa mafunzo mawakala wetu ili kutoa huduma za msaada inavyowezekana. Daktari alieleza.
Tangazo hili linakuja muda mchache tu baada ya vyuo vikuu(colleges) kuanza kusambaza barua za Kuwaita Wanafunzi barua zaidi ya 14,338 za wanafunzi walioteuliwa kujiunga na vyuo katika awamu ya mwezi wa tatu.
Daktari Oluoch alidhibitisha kuwa barua za kusajiliwa kwa ngazi ya kujiongeza masomo ikiwemo na kiwango cha stashahada (Diploma) stashahada ya juu(higher Diploma) na programu za masomo ya astashahada(certificate) zitaendelea kutolewa .
Kozi mbalimbali zinawezapatikana katika mitandao ya mtambo wa wanafunzi katika students.kuccps.net/programmes /sea.
Kozi hii ya utabibu ni kozi mojawapo muhimu sana katika taaluma mbalimbali hivyo lilikuwa ni jambo la busara kwa taasisi husika kutoa mwanya na melekezo ya kuwapanga na kuwatuma wanafunzi katika vyuo mbalimbali ili kusaidia katika kutibu na kutoa huduma za aftya kwa jamii.
Vilevile kutokana na kuwa sekta ya afya iliweza kugatuliwa na kuwa chini ya usimamizi wa serikali za Kaunti hili ni jambo ambalo limeleta mwangaza katika sehemu zetu za mashinani kwa kuwa matabibu wako na wanapatikana kwa wepesi .
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!