
MSANII wa Konde Music Worldwide, Harmonize ameonesha nia ya kutaka kukutana na aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz.
Wasanii wengi wako katika kisiwa cha Zanzibar ambapo kunatarajiwa kufanyika hafla ya tuzo za Trace Jumatano hii.
Harmonize alikuwa na mshawasha wa kukutana na Diamond baada ya kufika visiwani Zanzibar na kushangaa kuona msafara wa magari ya Diamond kwenye eneo la maegesho.
Harmonize alijiuliza maswali mengi kuona magari ya Diamond yakiwa na nambari binafsi za usajili ‘SIMBA’ huku akibaki kujiuliza ni vipi magari hayo yaliweza kuvuka kutoka bara hadi kisiwani humo mbele ya kuwasili kwake.
Alisema kwamba kutoka kwa Diamond, amejifunza mengi, haswa jinsi ya kufanya muziki kibiashar,a na kutaka kukutana naye wakiwa huko Zanzibar.
“Najivunia wewe kaka yangu. Nafikiri nimejifunza mengi kuhusu showbiz. Nawaza haya magari yamefikaje huku. Yamepaa au yameogelea? Uko serious sana na kazi yako, ningependa kukutana na wewe,” Harmonize aliandika.
Tamasha la kutolewa kwa tuzo hizo litafanyika katika mgahawa mmoja kisiwani Zanzibar usiku wa leo ambapo Diamond kando na kuteuliwa kuwania tuzo hizo, pia atakuwa mmoja wa wasanii watakaotumbuiza kabla ya kutolewa kwa tuzo rasmi.
Wasanii wengi wa Tanzania walionesha picha na video jinsi walitua katika visiwa vya Zanzibar, Nandy akiweka unyonge wake pembeni na kuvutia wengi kwa jinsi alivyotua kwa ndege ya kibinafsi kabla ya kusindikizwa hotelini na msafara mkubwa wa magari yenye haiba iliyotukuka.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!