
MSANII Kevin Kioko maarufu kama Bahati amewashauri wanaume wasio na pesa kuepuka kabisa suala la mapenzi.
Akichukua kwenye ukurasa wake wa Instagram alikofichua zawadi nambari 6 kati ya nane ambazo alianza kumpa mkewe wiki iliyopita kama njia moja ya kusherehekea miaka 8 ya ndoa yao, Bahati alisema kwamba mapenzi na kuchumbiana si vitu vya watu wasio na pesa.
Kwa mujibu wa msanii huyo, mwanamume yeyote anayetaka kupenda na kupendwa sharti awe tayari kumtumia pesa zake kumfurahisha na kumpendezesha mwanamke wake.
Alisema kwamba yeyote asiyetaka kumtumia pesa zake kwa mwanamke, au mwenye hana pesa basi mapenzi hayamfai, na aghalabu hao ndio huwakosea warembo heshima kwa kuwaita ‘gold diggers’.
‘Wapendwa Wanaume; Ushauri wa heshima ? Kama huna Pesa Usichumbie ? Ndio Njia Pekee Utakayoacha Kuwaita Wanawake Wachimba Dhahabu ? Kwenye Post Yangu Inayofuata Nitakuonyesha ni kiasi gani nilichotumia kwa Zawadi ya Mke Wangu NO.6 Vito vya Wapendanao,” Bahati alisema.
Kwa takribani wiki mbili, msanii huyo amekuwa gumzo la mitandaoni kutokana na haiba za zawadi ambazo amekuwa akimkabidhi mke wake, Diana Marua.
Bahati alianza kumpa mkewe zawadi kama vile mashamba, mradi wa ujenzi wa nyumba za kuishi miongoni mwa zawadi zingine kusherehekea miaka 8 ya uhusiano.
Wiki iliyopita, Bahati alijitoa kimasomaso kuchorwa tattoo ya jina la ‘Diana B’ kwenye mkono wake kabla ya kumpa Diana Marua zawadi zingine.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!