
MWANAMKE mmoja mwenye umri wa makamo amezua gumzo katika mitandao wa X baada ya kuibua tetesi kwamba wanaume wanaojua kupika kuwa nao katika mahusiano ni kujikosea heshima kama mwanamke.
Katika video hiyo ambayo imegawanya wachangiani maoni kwa makundi mawili, Mrembo huyo alianza akisema kwamba anawaonea huruma sana wanawake walioko kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanaume ambao ni wapishi wazuri.
Kwa mjibu wa mwanadada huyo, mwanamume yeyote ambaye ni fundi katika masuala ya jikoni ni ‘red flag’ kubwa sana, akisema kuwa hao mara nyingi ndio huwa sumu kuishi nao.
“Unapoolewa na mwanamume anayeweza kupika ni red flag. Wakati nyinyi mnapigana, atapika, atakula, atafurahi na kwenda kulala.”
“Hakuna kisingizio cha yeye kukubembeleza. Hasa ikiwa anaweza kupika zaidi yako na pia kujua jinsi ya kuweka ubaya, utateseka katika uhusiano huo,” alisema.
Aliongeza akitoa onyo kwa wanawake kutofanya uthubutu wa kuolewa na mwanamume anayejua kupika, akiita hatua hiyo kama moja kati ya makosa makubwa ambayo mwanamke yeyote anayejipenda atafanya.
Mwenyewe, alisema kuwa hawezi kubali posa kwa mwanamume anayejua kupika hata kwa mtutu wa bunduki.
“Usijaribu kuingia katika uhusiano na mwanamume anayejua kupika, hata mimi mwenyewe siwezi kubali mwanamume wangu awe hodari jikoni. Kupika ni biashara yangu tu,” aliongeza.
Tazama video hiyo hapa chini jinsi watu waliweza kuchangia maoni kwenye jambo hilo;
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!