Morara Kebaso

MWANAHARAKATI Morara Kebaso amefichua kwamba biashara zake zilimuingizia takribani milioni 140 katika mwaka wa 2024 pekee.

Akizungumza kwenye podikasti ya Dr King’ori, Kebaso alisema kwamba mapato hayo ni kutokana na biashara zake za kuuza samani na zingine ndogo ndogo.

Kiongozi huyo wa chama cha INJECT alisisitiza kwamba mapato hayo yalitokana na biashara zake tu na wala hayajumuishi hela za michango ambazo alipokea kutoka kwa watu mitandaoni kwa ajili ya kuendesha harakati za kutoa elimu ya kiraia katika Maeneo mbalimbali.

“Mapato yangu kwa mwaka 2024 yalikuwa takribani shilingi milioni 140. Hii ni pesa kutoka kwa biashara zangu, michango ya Gen Z hata haifiki huko,” Kebaso alisisitiza.

Kuhusu chanzo cha mapato yake, Kebaso alisema kwamba baada ya kufanya kazi kama wakala wa kuuza fenicha, hatimaye alianzisha karakana yake ya kujiundia fenicha na kuuza.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kisha baadae akanunua gari la kifahari alilolitumika kukodishia watu kwa ajili ya ziara mbalimbali, akisema kuwa alilinunua kutokana na mkopo wa benki huku akishauri watu kuwa na mlahaka mwema na benki badala ya kuweka akiba kwenye M-Pesa.

Kebaso alisisitiza kwamba yeye alianza kujitengenezea hela ndefu muda mrefu nyuma hata kabla ya kujitambulisha kwa Gen Z kupitia vipindi vyake vya ‘Vampire Diaries’ ambapo alikuwa anatumbua miradi ya serikali iliyokwama.