
Mchungaji Lai ahubiri kuhusu maadili
Willifred Lai mchungaji wa kanisa la Jesus Celebration Centre liliko Bamburi Mombasa alihubiri kuhusu ufisadi,wizi naa kiburi miongoni mwa Viongozi.
Katika Mahubiri yaliohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini akiwemo Rais Ruto, mchungaji Lai aliweza kuwahubiria waumini kwa kuwaeleza maovu ambayo hutendwa na binadamu duniani.
Mchungaji aliweza kuhubiri kwa mafumbo huku akiashiria kuwalenga watawala ambao hutumia nafasi na hadhi zao kuwadhulumu wanyonge kwa kutangaza sera za uongo na kutowajibika ipasavyo.
Mchungaji Lai kulingana na mujibu wa mahubiri yake aliweza kusema kuwa viongozi wale ambao wanaeleza sera za uongo na kula mali ya umma hawatafanikisha malengo yao bali watafariki kabla ya kutimiza kile ambacho walikidai kama kuendeleza ajenda za uongo na ufisadi.
Mchungaji Lai alisema Viongozi ambao wanadhani kuwa kukuwa tajiri ni lazima uwe fisadi na uwaibie raia au wananchi alisema kuwa kwa kufanya hivyo walikuwa tayari wamelaaniwa na kumuibia Mungu kwani ufalme wa Mungu si wa wanyang’anyi.
Wakati ambapo mchungaji alikuwa anahubiria waumini waliokuwa kanisani walionekana kuchangamkia kauli na mahubiri ya mchungaji wakisema kuwa yalikuwa ni mahubiri na injili kali na takatifu amabayo ilikusudia kuwanyoosha wale ambao walikuwa na mienendo potovu wabadilike.
Injili iliweza kujikita katika masuala ya ufisadi, kiburi, majigambo na maringo mchungaji akishauri wakristo kubadilisha mienendo yao hasi ambayo haimufurahishi Mungu, mchungaji alionekana kuwalenga wakiristo mbalimbali ambao wamekuwa wacha Mungu ila mara nyingi wamekuwa na tabia kama za Lumbwi.
Injili ya aina hii ilikuwa ikiendelezwa na watumishi wa Mungu kila mahali wanapokutana ili kuwawosia viongozi kujali na kuhudumia wananchi kwa kutimiza ahadi walizo ahidi wananchi.
Itakumbukwa kuwa askofu bwana Antony Muheria kwa wakati mmoja alinukuliwa akitoa matamshi ya kuishauri serikali iweze kutekeleza wajibu wake kwa kumhudumia mwananchi kwa uzalendo wa hali ya juu.
Wosia wa bwana Muheria ulipokelewa kimseto na baadhi ya viogozi serikalini waliomkashifu kwa kuasi mambo ya dini na kuingilia siasa za taifa wakimtaka ajiuzulu na ajitose siasani bila kuogopa
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!