
MUIGIZAJI wa Nollywood, Regina Daniels mwenye umri wa miaka 24 amewatupia bomu la neno zito watu wanaokejeli ndoa yake kwa bilionea Ned Nwoko mwenye umri wa miaka 64.
Regina ambaye alifunga akaunti yake ya Instagram wiki iliyopita baada ya uvumi kuzagaa kwamba mumewe alikuwa amepachika mimba muigizaji mwingine alienda kwenye TikTok kutuma ujumbe huo kwa watesi wake.
Hii ni baada ya kupata pumzi jipya wakati Nwoko alibainisha wazi kwamba habari za yeye kumpachika mimba muigizaji Chika Ike ni za uwongo.
Regina alichapisha video akiwa amevalia vazi jekundu akitembea kueleka kwa gari lake jekundu aina ya Ferrari na kuwafokea wanaodhihaki ndoa yake kwamba wasiendelee na umbea huo ikiwa hawajawahi lia ndani ya gari la kifahari kama hilo.
Pia aliwaambia watu kama hawawezi kumudu bei ya vazi kama hilo lake, ni vyema kunyamaza badala ya kuendeleza masengenyo kuhusu ndoa yake na bilionea Nwoko.
“Usitoe maoni ikiwa hujawahi kulilia ndani ya Ferrari na toa Maoni ikiwa unafaa kumudu kitambaa hiki,” alichapisha.
Kwa miaka iliyopita, Regina na Nwoko wamekuwa wakionyesha mapenzi yao hadharani kupitia mitandao ya kijamii, hasa wakati wa sherehe muhimu kama Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day).
Hata hivyo, mwaka huu hakukuwa na ishara yoyote ya kusherehekea siku hiyo, hali ambayo iliwafanya mashabiki wake kuanza kuhisi kuwa huenda kuna matatizo katika ndoa yao.
Hii haikuwa mara ya kwanza jina la Chika Ike kuhusishwa na bilionea huyo kwani mnamo 2020, kulikuwa na madai kuwa wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini Chika alikanusha vikali uvumi huo, akisisitiza kuwa hana mpango wa kuwa mke wa Nwoko.
Hata hivyo, ujauzito wake wa sasa umefufua mjadala mpya kuhusu uhusiano wao, huku mashabiki wakitilia shaka hali ya ndoa ya Regina, na kuchochewa zaidi na hatua ya Mrembo huyo kufunga ukurasa wake wa Instagram.
Hata hivyo, siku 5 zilizopita, bilionea huyo alilaza uvumi wote kitandani na kuwaacha na tope nyusoni wambea waliokuwa wakimhusisha na mimba ya Chika Ike.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!