
MWANAMKE mmoja ambaye ni mtengenezaji wa maudhui amezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii baada ya video yake akilipia huduma kuoshwa kwenye kituo cha kuosha magari kusambaa mitandaoni.
Katika video hiyo, mwanamke huyo aliyekuwa amevalia rinda la kahawia alielekea kwenye kituo cha kuosha magari ambapo aliwapata vijana wawili wakiwa katika harakati za kuosha gari moja.
Kwa wakati huu wote, alikuwa anashikilia simu yake kwa mkono mmoja huku akirekodi na kutumia mkono mwingine kuchomoa Burunguti la hela kutoka kwa mfuko wake.
Kisha aliwauliza wale vijana wangemlipisha kiasi kipi kwa huduma ya kumuosha kama vile gari, swali ambalo kwa sekunde kadhaa liliwashangaza vijana wale.
Kisha baada ya kukubaliana bei, alimkabidhi mmoja wao hela na kuwaamrisha wamuoshe kuanzia kichwa hadi wayo kwa sabuni na maji, mithili ya gari – huku akirekodi tukio zima.
Vijana wale maadamu wameshapokea pesa, walianza mchakato wa kumuosha kuanzia kichwani hadi miguuni huku Mrembo huyo alijirekodi licha ya pofu jingi la sabuni kugubika uso wake.
Tukio hili lililizua mjadala mkubwa, huku wengi wakihoji hali ya ubunifu katika kutengeneza skit.
Mcheshi maarufu wa Nigeria Klinton Cod alichapisha tena video hiyo, akilaani kitendo hicho na kuwakosoa watengeneza maudhui wakuu kwa kuidhinisha maudhui kama hayo.
Alisikitika kudorora kwa viwango vya ubunifu ndani ya tasnia hiyo na akapendekeza watayarishaji wa maudhui wasajiliwe na kupewa leseni ili kukabiliana na kile alichokitaja kuwa kero inayoongezeka.
Akikubaliana na maoni ya Klinton Cod, mtumiaji wa mitandao ya kijamii @alsinasteve alijibu, "Tunapoteza maadili yetu tangu mitandao ya kijamii ianze kuwalipa watu…wanaweza kufanya chochote kwa ajili ya pesa na umaarufu."
Mtumiaji mwingine @justice_crack aliongeza, “Ninaamini mapinduzi yanakuja katika tasnia ya uundaji maudhui. Ikiwa sote tutaendelea kutangaza maudhui mabaya, tasnia yetu ya uundaji wa yaliyomo itabadilika na kuwa bora kwa wakati.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!