Ni Juma ambalo tutashuhudia hatima ya majaji ikiwa kesi mbalimbali zilizowasilishwa kortini zitasikilizwa na kuamuliwa.

Lakini hilo likisubiriwa viongozi mbalimbali walijitokeza  kuwatetea majaji hao  na wengeni kusema hilo si jambo la kuzungumziwa waziwazi.

Hapo jana Jumapili, aliyekuwa naibu wa rais bwana Rigathi Gachagua akiwa katika Kaunti ya Meru aliweza kutoa madai kwa kusema kuwa kuna mpango unaosukwa na serikali kuwaondoa majaji saba wa mahakama ya upeo ofisini.

Katika matamshi yake Bwana Gachagua aliweza kusema kuwa ana ufahamu wa mpango maalum ambao ulikuwa unapangwa na kuendelezwa na rais Ruto  wa kuhakikisha kuwa Jaji mkuu Koome anaondolewa afisini pamoja na majaji   wengine sita.

Gachagua alionekana akimtaja kwa jina Rais Ruto akimuonya kuwa ikiwa ataruhusu jambo kama   hilo bila shaka atakuwa amekataka uhusiano wake na watu wa mlima kenya hasa Meru

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Gachagua alikuwa akiwaeleza wananchi hao kadamnasi huku akiwaahidi kuwa iwapo rais atajihusisha na mchakato huo bila shaka atakuwa ameyakaribisha maandano makubwa ambayo Gachagua alisema huenda atayaongoza.

Kwa upande mwingine Waziri wa usalama wa ndani Bwana Kipchumba Murkomen alionekana kukashifu matamshi ya Gachagua akimkumbusha kuwa afisi za majaji Pamoja na majukumu yao na adhabu inapohitajika huwa inafuata  mkondo maalum tena  wa kisheria ambao haupingiki na na huwa hauingiliwi kwa misingi ya kikabila bali kwa misingi ya sheria na kazi.

Kauli ya Murkomen ilijiri punde tu baada ya Gachagua kuzungumza akimtetea bi Koome, Murkomen alisema kuwa majaji wana njia yao ya kikatiba na hufanya kazi kwa kuchagukiwa  bali si kwa misingi ya ukabila.

Hatimaye Naibu wa Rais Kithure Kindiki kwa namna moja pia aliandika katika ukurasa wake wa X akisema kuwa kuondolewa kwa majai au Jaji ni jambo la kikitiba bali si la kisiasa.

Alieleza kuwa iwapo una shida na jaji au majaji kuna tume maalum kisheria iliyo na majukumu maalum kikatiba kutekeleza wajibu huo bali si kulihusisha jambo hilo na ukabila ndani.

Alifafanua akisema kuwa kukosoa majaji lazima kuwe kumejikita katika misingi ya kisheria na kwa kufuata sheria si ukabila.

Itakumbukwa vyema kuwa zipo kesi nyingi ambazo ziliwasilishwa na wakili Havi na Ahmednasir Abdullahi wakitaka majaji hao wote waondolewe afisini kwa madai ya usifisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.