Gen Muhoozi Kainerugaba, Winnie Byanyima

WINNIE Byanyima, mke wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye na ambaye anatajwa kuwa mpenzi wa zamani war ais Yoweri Museveni amemuonya mwanawe rais huyo, Muhoozi Kainerugaba dhidi ya kuzungumzia uhusiano huo wa zamani, akisema hajui chochote.


Kupitia ukurasa wake wa X, Byanyima alimuonya Muhoozi dhidi ya kukurupukia na kupayukia suala la uhusiano wake wa zamani na Museveni, akisema kwamba ni uhusiano uliokuwa changamano zaidi na ambao wote – yeye na Museveni, waliamua kuutupa katika kaburi la sahau na kila mmoja kujishughulisha na ya kwake.


"@mkainerugaba IWE MWANA WE…. Yetwaare. Ninahisi ni muhimu kuwa wazi: Kuna historia ngumu zaidi kati ya baba yako na mimi ambayo sote tumechagua kuvuka kwa kuheshimiana," Byanyima alichapisha kwenye X.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Winnie alimuonya Muhoozi zaidi akisema kwamba ikiwa ataendelea kuzungumzia uhusiano wake wa zamani na Museveni basi itambidi atoe ukweli mgumu ambao utamchanganya na kumfanya kujuta.


"Hata hivyo, ikiwa utaendelea kuwasilisha simulizi ya uwongo, huenda nikahitaji kutoa ushahidi MGUMU wa ukweli. Napendelea kudumisha mtazamo wetu wenye heshima, lakini chaguo hilo linabaki kuwa lako. Ninaona kuwa suala hili limefungwa."


Jenerali Kainerugaba, ambaye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, alienda kwa X kusimulia jinsi uhusiano kati ya Museveni na Byanyima ulivyomalizika.


Muhoozi alitoa tamko lake saa chache baada ya Winnie kudai kwamba katika kitabu chake kijacho, atasimulia kwa sehemu kuhusu uhusiano wake wa zamani na Museveni kabla ya kuachana na kuoana na Besigye.


"HAKUNA kitu cha kawaida katika uhusiano wako na baba yangu. Ulipata nyumba yenye furaha ukajaribu kuibomoa. Wewe ni MSIBA wa mwanamke!! Hukutoka. Mzee alikufukuza nyumbani Desemba 1986, akakuburuza hadi kwenye gari huku unalia na kukupeleka kwa wazazi wako."


Kabla ya kufunga ndoa na Dk Kizza Besigye Julai 7, 1999, huko Nsambya, Kampala, Byanyima alikuwa akihusishwa kimapenzi na Museveni. Yeye na Besigye wana mtoto wa kiume, Anselm Besigye, ambaye kwa sasa anafuata PhD katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York.