Serikali ya Sudani iliikosoa vikali serikali ya Kenya kutokana na hatua yake ya kulikaribisha kuundi la waasi wa RSF kutia Saini ya makubaliano na washirika wao jijini Nairobi.
Katika taarifa rasmi iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Sudani ilisema kuwa hio ni uvunjaji wa wajibu wa Taifa la Kenya chini ya sheria za kimataifa,mkataba wa umoja wa mataifa ,misingi ya umoja wa Afrika na mkataba wa kuzuia uhalifu wa kimbari.
Sudani ilidai kuwa Kenya ilikiuka ahadi yake ya kuzuia shughuli za uadui dhidi ya Sudani kutoka katika ardhi yake.
‘’Hatua hiyo ya serikali inapinga kanuni za ujirani mwema vilevile inakwenda Kinyume na ahadi zilizotolewa na Kenya katika ngazi ya juu ya kutoruhusu shughuli zozote kufanyika katika ngome yake taarifa hiyo ilieleza’’.
Serikali ya Sudani ilipuzilia mbali madai ya kuwa shughuli za RSF jijini Nairiobi hazikuwa na mashiko yoyote na kutaka jamii ya kimataifa kulaani kitendo hicho.
Wanamgambo wa RSF wamekuwa na mzozo na serikali tawala ya Sudani na mara kwa wamekuwa wakitishia kuuunda serikali mbadala ndani ya Sudan wakisema kuwa shughuli hiyo ingefanyikia jijini Nairobi.
Makubaliano ambayo RSF na makundi husika yalikusudia yawe na maafikiano ya utendakazi wa kudumu ikizingatiwa kuwa makundi ya washirika wake ambayo yana silaha yalilenga kuunda serikali mbadala ya Amani na Umoja katika maeneo ambayo RSF inadhibiti.
Walitoa madai kuwa makubaliano na washirika wao wa karibu yalilenga utoaji wa huduma za afya,ulinzi,na kuwa na uhalali wa kuendesha shughuli zao bila matata.
Hata hivyo washikadau ambao wanahusika na mchakato huo wa utekelezaji wa mkataba huo hawakueleza makubalianao hayo yalikusudia nini ila kamati husika iliwahi sema kuwa lengo lao lilikuwa ni kurejesha serikali halali ambayo ilipinduliwa na wanamgambo wa kiislamu.
Kulingana na wao walisema hiyo ilikuwa njia moja wapo ya kujumuisha kila mmoja katika serikali ambayo itakuwa ya umoja na amani kwa uwendelevu hivyo wengi wanaliangazia suala hilo kwa ukaribu kutaka kujua ni nini kitachofuata.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!