Gavana Sakaja apongeza programu ya lishe kwa watoto shuleni

Mpango wa programu ya lishe shuleni ambao ni mradi ulioasisiwa na Gavana Johnson Sakaja ulipigiwa upato na kuonekana  kuwa wa manufaa sana.

Programu hio ambayo ilipewa jina maarufu ‘Dishi na Kaunti’ ni programu ambayo ilikusudiwa kuwapa mlo wanafunzi  wa shule za umma kwa gharama ya chini sana katika maeneobunge kumi na saba(17)  Nairobi.

Kutokana na kuanzishwa kwa mradi huu muhimu wa maankuli shuleni umechangia pakubwa kujengwa kwa jikoni kumi na saba na kuwaajiri wafanyakazi wengi katika mpango huo.

Huu mradi ni miongoni mwa miradi ambayo ilikuwa katika manifesto ya Gavana alipokuwa akirai wananchi wampigie kura akisema kuwa ni mradi ambao ulilenga shule za umma zote zikiwemo za chekechea.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

‘’Dishi na Kaunti ni ndoto ambayo imekuja kutimia nikiwa Seneta nilitamani sana kuona Watoto wakila shuleni kwa sababu nilibaini kuwa kati ya watoto wanne mtoto mmoja hukosa kuhudhuria Vipindi vya masomo kisa na maana ya ukosefu wa Chakula’’.

‘’Niliahidi kuwa iwapo nitachaguliwa ningeanzisha mradi huo kwa haraka iwezekanavyo na kwa sasa ninaona hilo limetimia ambapo ni jambo zuri la kujivunia’’Gavana alisema.

Kwa sasa mpango huo wa Dishi na Kaunti unalisha jumla  ya Wanafunzi elfu mia tatu na Watoto kumi 310,000 nambari ambayo ni ya kujivunia na ambayo inaashiria mwanga wa maisha mema kimasomo kwa wanafunzi wetu wawapo shuleni.

Mradi huu wa Gavana ulilenga kupunguza baa la njaa kwa wanafunzi hasa wa mijini ili kuwapa nafasi sawa kimasomo na kupata elimu pasi  kuwa na vikwazo vyovyote.

Gavana anapoendeleza mipango ya ajenda yake katika jiji kuu la Nairobi hio ni baadhi tu ya miradi imara ambayo amekuwa akiendeleza ikiwemo na shughuli ya kulisafisha jiji la Nairobi na kuwaondoa wachuuzi Katikati ya jiji kuu.

Gavana awapo mbioni kutimiza ahadi zake alizowaahidi wananchi wa Nairobi vilevile ameendeleza wito wa kuwa na ushirikiano kati ya maafisa wa mamlaka inayosimamia shughuli na kuendesha mipango ya Nairobi na wananchi ili kuwe na wepesi wa kutekeleza na kufanikisha shughuli za Kaunti  pasi kuwa na mvutano wowote .