Naibu  wa rais Kithure Kindiki akihutubia viongozi kutoka Kaunti ya Meru

Naibu wa rais Profesa  Kithure Kindiki alikutana na viongozi na wananchi kutoka Kaunti  ya Meru kujadili masuala ya maendeleo.

Naibu wa rais huyo aliandaa kikao hicho katika makao yake ya Karen jijini Nairobi ambapo viongozi mbalimbali wa ngazi tofauti walihudhuria kwa manufaa ya ushirikiano na utangamano wa kitaifa na hata kimashinani.

Naibu wa raisi alieleza  ajenda ya mkutano huo akisema kuwa ilikuwa siku ya kujadili maendeleo katika kaunti ya Meru kile ambacho viongozi walikuwa wanakusudia kitendeke na ambacho walikuwa wanapendelea kiwekwe kama ajenda muhimu tena ya kushughulikiwa na serikali kuu.

Kati ya miradi ya maendeleo ambayo ilijadiliwa ni kukarabati na kutamatisha miradi ya maendeleo ambayo ilianzishwa na ambayo  haijakamilika kama Barabara,sekta ya  kilimo,biashara ya zao la miraa miongoni mwa mengine mengi.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Naibu wa Rais akizungumza katika mkutano huo alidadavua vyema na kuelezea hatua za maendeleo ambazo serikaali imetekeleza kwa muda wa miaka miwili ambayo imekuwa madarakani.

Kindiki alieleza kuwa wakati ambapo serikali ilichukua hatamu za uongozi hali ya Uchumi haikuwa ikifanya vizuri akasema kuwa kulikuwa na janga la uviko 19 (covid 19) ukonjwa ambao ulisambaratisha Uchumi kabisa na kufanya hali ya maisha kuwa mbaya zaidi.

Katika kipindi hicho dola ya marekani ilinunuliwa kwa shilingi 165 pesa za Kenya jambo ambalo lilidhoofisha sana Uchumi wa nchi vilevile alieleza kuwa biashara hazikukuwa zikifanya vyema jambo ambalo lilifanya biashara nyingi kufunga,na hata kuathiri sekta ya uchukuzi.

Enzi hizo kulikuwa na ugumu wa maisha kwa wengi hivyo wananchi kupata chakula ilikuwa vigumu akieleza kuwa kilo mbili ya unga wa ugali  iliuzwa shilingi mia 250  jambo ambalo liliwawia vigumu wananchi kuweka ugali kwa meza.

Profesa Kindiki alielezea juhudi ambazo serikali imekuwa ikipiga  kuhakikisha kuwa inarudisha hali ya Uchumi katika mkondo mwema kwa kuhakikisha kuwa Uchumi unakua na gharana ya mafuta inapungua ili kumwauni mwananchi wa kipato cha chini.

Vilevile katika mkutano huo Naibu wa rais aliwaeleza viongozi hao kuratibu chini miradi ambayo wangependa serikali ishughulikie baada ya kutamatisha miradi ambayo imekwama kwa sasa Naibu wa rais akiwarai viongozi wa Meru kwa jumla kuunga mkono serikali kwa manufaa ya maendeleo ya eneo hilo.