
Viongozi wa bara la Afrika katika ukumbi wa Nelson Mandela Ethiopia.
Baada ya kipindi cha uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa AUC kutamatika, baadhi ya wachanganuzi wa masuala ya diplomasia na kisiasa wametoa sababu za Kenya kupoteza katika uchaguzi huo.
Wachanganuzi mbalimbali wamejitokeza na kuweka bayana baadhi ya masuala ambayo huenda kama taifa hayakutiliwa maanani na kusababisha mwaniaji wa Kenya kufeli.
Seneta Richard Onyonka ambaye pia ni mtaalamu katika masuala ya kidiplomasia alipohojiwa na kituo kimoja cha Habari nchini ili aeleze kwa maoni yake chanzo kilichosababisha Kenya kupoteza katika uchaguzi wa AUC.
Bwana Onyonka alifafanua kuwa sababu ya kwanza ambayo ilichangia Kenya kupoteza katika kinyang’anyiro hicho ni kuwa na sera potovu za kidiplomasia kuhusu siasa zetu za kikanda na masilahi ya mataifa mbalimbali duniani.
Vilevile alifafanua wazi kwa kusema kuwa Vita katika taifa la Jamhuri ya Kongo pia vilichangia pakubwa ambapo rais William Ruto ndiye mwenyekiti wa ukanda wa Afrika Mashariki (EAC),alipoitisha mkutano wa Pamoja kushughulikia suala hilo ilishangaza rais wa Kongo hakuhudhuria mkutano huo.
Kutokana na rais wa Kongo bwana Felex Tsisekedi kususia mkutano wa ukanda wa Afrika Mashariki na kuhudhuria ule wa SADK ilikuwa ni ishara kuwa mambo hayakuwa yanaendelea vyema kutokana na suala la kuleta amani katika taifa lake la Kongo.
Inasemekana kuwa pia katika matamshi ya rais William Ruto miezi kadhaa iliyopita kuhusu vita vya Israeli na Palestine alinukuliwa waziwazi rais Ruto akipongeza taifa la Israeli na kuahisi Palestine usemi ambao haukuchukuliwa vyema na viongozi ambao wanaegemea dini ya kiislamu.
Jambo ambalo lilichochea mataifa yanayoegemea dini ya kiislamu kuchukua mkondo tofauti na kumpigia kura mwaniaji wa Djibout Mohamoud Ali Youssouf ambaye alikuwa mwisilamu,kutokana na kigezo hiki viongozi wengi wa mataifa mbalimbali waliamua kuchukua misimamo yao tofauti.
Wakili PLO Lumumba katika maoni yake alieleza kuwa kuanguka kwa Raila katika kiti cha uenyekiti wa AUC si wa binafsi bali ni wa Taifa kwa jumla, kwani hiyo iliashiria tabia na sura ya taifa katika nchi za nje.
Vilevile alieleza kuwa ni kutokana na kufeli kwa kitengo cha masuala ya diplomasia kutofanya urafiki wa karibu uhusiano mwema na mataifa mengine ya nje akisema kuwa huo sasa ndio mwamko mpya wa kujenga uhusiano mwema na mataifa ya nje na kuteua watu bora zaidi.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!