
Mwanaume mwenye umri wa miaka 40 amehukumiwa kifungo cha miaka 150 jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua watoto wake watatu.
Muhusika alitiwa mbaroni mwaka 2019 baada ya kutekeleza mauwaji hayo katika eneo la Lelaitich, kaunti ya Bomet na kesi hiyo imekuwa ikiendelea.
Wakati akitoa hukumu hiyo leo Jumatatu, Jaji wa Mahakama Kuu ya Bomet Julius Kipkosgei Ng'arng'ar alipitisha hukumu hiyo huku kila kesi ya mauwaji ya mtoto mmoja ikiidhinisha kifungo cha miaka 50. Idadi ya miaka ya kufungwa ikajumuishwa na kuwa 150 kutokana na hatia ya kuwauwa watoto watatu, hatia ambayo amepatikana nayo.
Benard Kipkemoi Kirui alipatikana na hatia ya kuwaua wanawe watatu; Amos Kipngetich mwenye umri wa miaka 12 Vincent Kiprotich niaka nane na Emanuel Kipronoh miaka 5.
Mhusika alitekeleza kitendo hiki kiovu wakati mama yao alikuwa mbali na nyumbani.
Sharon Cherono, mama wa marehemu, alipongeza uamuzi huo na kuishukuru mahakama kwa kuhudumia haki kwa watoto wake.
Jaji Kipkosgei alitaja mauaji hayo kuwa ya kikatili na ya kinyama na kwa hivyo hukumu hiyo itatumika kama mfano kwa wale wenye nia ya kutenda uhalifu kama huo.
Hata hivyo, alisema kuwa Kirui ana siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Kosa la kuuliwa kwa watoto na wazazi wao limekuwa la kusitusha humu nchini. Swala hili likiwakaba wazazi wa kiki na kiume wote.
Wiki Jana mwanaume mmoja alipoteza familia yake yote baada ya mkewe kuwauwa wototo wao watatu na baadaye kujiangamiza kulingana na ripoti ya polisi. Hali sawia ilitokea mwaka jana 2024 baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 35 kutoka kauti ya Bomet, aliwauwa wanawe wawili kabla ya kujiondoa uhai.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!