Afisi ya mkurugenzi mkuu wa mashitaka ya umma ODPP iliandika barua kuelezea madai ya afisa mkuu mmoja wa serikali aliyedaiwa kujihusisha na kitendo cha hongo ya shilingi 50,000.

Katika barua ambayo ilitumwa kwenye mitandao ya kijamii tume hiyo ya afisi ya mkurugenzi wa mashitaka ya Umma ODPP ilieleza kuwa kulingana na sheria za utendakazi wa haki na usawa kwa wote hakuna afisa Yeyote wa serikali au umma ambaye ana haki ya kuvunja sheria.

Kulingana na madai yaliyoibuliwa imesemekana kuwa afisa mmoja wa ngazi ya juu kazini alipokea rushwa ya shilingi elfu Hamsini kutoka kwa mfanyabiashara mmoja ili kusitisha mchakato wa kupelekwa kortini.

ODPP ilieleza kuwa kulingana na sheria yao ya utendakazi hamna afisa yeyote wa serikali ambaye ana haki ya kupokea rushwa kwa misingi ya kuwa yeye  mkubwa au anaitumikia serikali, barua hiyo ilisisitiza kuwa tume hiyo imejikita katika mashitaka yenye haki na usawa.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Kwa hivyo afisi ya mkurugenzi mkuu  ODPP  ilitoa mwelekeo afisa ambaye alihusika ambaye jina lake halijawekwa wazi asimamishwe kazi aanze likizo ya lazima huku akipisha uchunguza kuanza kwa upesi.

Barua hiyo ilieleza ikinuku kipenge cha utendakazi kinachofafanua haki za kila mfanyakazi anapokuwa kazini kile ambacho hastahiki kujihusisha nacho na kile ambacho anastahili kufanya.

Afisi hiyo ilisisitiza ikieleza kuwa ingeshirikiana na asasi nyingine za sheria ili kuhakikisha  kuwa wavunja sheria wanakabiliwa vilivyo na mkono wa sheria.

Kwa kipindi kirefu sasa hiyo tume imekuwa mbioni kukabili na kuchunguza vitendo vya wakenya mbalimbali vya  kujihusisha katika visa vya ulaghai,utapeli na hongo kwa kutumia mamlaka yao au nafasi zao kama wafanyakazi wa serikali.

Tume hiyo ilidadavua ikisema kuwa hamna yeyote angesazwa kwa kigezo au misingi ya kuwa yeye ni afisa wa serikali au ana ukuruba na mkubwa Fulani.Kutokana na sheria ni kuwa haibagui mtu au watu kwa misingi ya matabaka na vyeo kazini.

Kulingana na hio barua ilitoa fursa ya kila mtu kutii sheria na kujiepusha na vitendo vya kushusha chini hadhi ya majina katika jamii vilevile tume hiyo ilifanya jambo la muhimu kuangazia kila hatua inayochukua ili tuwe na kizazi na jamii yenye maadili mema.